Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Derg
ni neno la Kiethiopia kwa ajili ya "kamati" au "halmashauri". Inamaanisha hasa kikundi cha wanajeshi waliompindua
Kaisari
Haile Selassie
mwaka
1974
na kushika mamlaka ya serikali nchini
Ethiopia
.
Derg ilikuwa kamati ya wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali za jeshi kama jeshi la nchi kavu, wanamaji, wanaanga na polisi.
Derg ilitawala hadi 1987.
Kati ya
1975
na
1977
watu makumi elfu waliuawa hovyo kwa amri za Derg.
Mwenyekiti na kiongozi mkuu wa Derg alikuwa
Mengistu Haile Mariam
.
1987
Derg ilikabidhi madaraka kufuatana na katiba mpya na Ethiopia kutangazwa kuwa jamhuri ya kisoshalisti na Mengistu rais wake.