Charles Scott Sherrington ( 27 Novemba 1857 ? 4 Machi 1952 ) alikuwa mwanafiziolojia kutoka nchi ya Uingereza . Hasa alichunguza neva za wanyama. Mwaka wa 1922 alipewa cheo cha "Sir". Mwaka wa 1932 , pamoja na Edgar Adrian alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba .