Charles Robert Darwin
(
12 Februari
1809
-
19 Aprili
1882
) alikuwa
mwanasayansi
Mwingereza
katika
karne ya 19
.
Amekuwa mashuhuri kutokana na
nadharia
yake ya
maendeleo ya uhai
(
mageuko ya spishi
).
Nadharia hii yasema kuwa
spishi
zote za viumbehai vimetokana na spishi asilia zilizogeuka baada ya muda. Mageuko haya hufuata
uteuzi asilia
yaani viumbehai wanaolingana vizuri zaidi na mazingira wanaishi na kuzaa kushinda viumbehai wasiolingana nayo.
Kwa njia hiyo tabia za viumbehai wanaofaa vizuri zaidi zinazidi kuendelezwa kwa sababu watoto wao hurithi tabia hizi. Lakini tabia za viumbehai wasiofaa sana zinaweza kutoweka kwa sababu wanakufa mapema na hawana watoto wengi wanaoendeleza tabia zao.
Alizaliwa mjini
Shrewsbury
(Uingereza) kama mtoto wa tano wa daktari Robert Darwin na Susannah Darwin (nee Wedgwood).
Baada ya kumaliza
shule
alijiunga na
chuo kikuu
] cha
Edinburgh
(
Uskoti
)
1825
akajiandikisha katika idara ya
tiba
lakini hakupenda
upasuaji
. Alitumia muda mwingi kufuata kozi za
biolojia
,
jiografia
na
jiolojia
nje ya masomo ya tiba. Alifuatana mara nyingi na wataalamu walipofanya uchunguzi wa wanyama, mimea au mawe.
Baba baada ya kuona hafai kuwa daktari alimwandikisha katika masomo ya
teolojia
kwa shabaha ya kuwa
mchungaji
wa
kanisa
la
Anglikana
aliyomaliza mwaka
1831
.
Baada ya kumaliza masomo haya Darwin alipata nafasi ya kujiunga kama mshiriki na safari ya kisayansi ya jahazi
MS Beagle
iliyotakiwa kuzunguka dunia yote kwa kusudi la kuboresha ramani hasa za pwani la
Amerika Kusini
. Darwin alipewa nafasi ya mwanaviumbe bila malipo ya kuongozana na kushauriana na
nahodha
na kiongozi wa safari kuhusu wanyama na mimea visivyojulikana na vitakavyopatikana safarini.
Katika safari hii Darwin aliona
Amerika Kusini
na visiwa vya
Pasifiki
. Akaona mengi na kushika kumbukumbu yake akakusanya mimea na miili ya wanyama na kuibeba naye kwa ajili ya maonyesho katika jumba la makumbusho la historia ya viumbe.
Kwenye visiwa vya
Galapagos
aliona ya kwamba kila kisiwa kilikuwa na
spishi
za ndege pia kobe zilivyotofautiana kidogo kati ya kisiwa na kisiwa.
Baada ya kurudi Uingereza mwaka
1836
Darwin alianza kuchunguza sampuli zote alizokusanya. Alipata kazi kama katibu wa shirika la jiolojia.
Alipochungulia sampuli za
Galapagos
hasa alipata dhana ya kwamba spishi hizi zote za karibu zilitokana na aina moja tu iliyowahi kufika kwenye visiwa hivyo lakini baadaye zilianza kuwa tofauti katika kila kisiwa na kuwa spishi ya pekee. Kama hiyo ilikuwa kweli spishi hizi hazikuumbwa hivyo tangu mwanzo.
Darwin aliendelea na utafiti wa sampuli zake na kutoa masomo mbalimbali na kuyatafakari.
1859
alitoa kitabu kuhusu
mageuko ya spishi
kwa njia ya
uteuzi asilia
(
On the Origin of Species by Means of Natural Selection, or the Preservation of Favoured Races in the Struggle for Life
) alimoeleza nadharia yake.
Kitabu kilikuwa kama bomu kati ya watu wa sayansi na wa dini.
Darwin alishambuliwa mara nyingi ya kuwa mafundisho yake yanapinga taarifa ya
uumbaji
katika
Biblia
. Lakini hiyo inategemea jinsi masimulizi yake yanavyosomwa: si lazima mwamini achukue kila kitu kama ilivyoandikwa, kwa sababu Biblia hailengi kutufundisha sayansi, bali njia ya wokovu.
Leo hii nadharia yake inakubaliwa na wanasayansi karibu wote hata kama bado kuna kiasi cha upingamizi dhidi yake kwa sababu za kisayansi na za kidini.