Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chama cha Mapinduzi
(CCM) ni
chama tawala
nchini
Tanzania
.
Historia
CCM ilizaliwa tarehe
5 Februari
1977
baada ya kuungana kwa vyama vya
Tanganyika African National Union
(TANU) kilichokuwa kikitawala
Tanzania Bara
na
Afro-Shirazi Party
(ASP) kilichokuwa chama tawala cha
Zanzibar
wakati huo. Chama cha TANU kilikuwa kikiongozwa na
Mwalimu Nyerere
na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya
Amaan Karume
.
Itikadi
Kwa miaka mingi CCM ilikuwa ikifuata
siasa
ya
Ujamaa na Kujitegemea
.
Itikadi
hii ilipewa nguvu za kisera mwaka
1967
lilipotangazwa
Azimio la Arusha
.
Kutokana na
azimio
hilo
uchumi
uliwekwa mikononi mwa
umma
. Itikadi hiyo pia ilisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja hasa katika
vijiji vya Ujamaa
.
Uchaguzi
CCM imekuwa ikishinda
chaguzi
za
Urais
toka
mfumo wa vyama vingi
uliporejeshwa nchini Tanzania.
Chama hicho kimekuwa pia kikipata
idadi
kubwa ya
wabunge
wa
Bunge la Muungano
na
Baraza la Wawakilishi
, ingawa
vyama vya upinzani
vilitoa malalamiko kuhusu utekelezaji wa
haki
na uchakachuaji wa
kura
.
Chaguzi za vyama vingi Tanzania baada ya kurejeshwa kwa mfumo huo zilifanyika mwaka
1995
,
2000
,
2005
na
2010
na viongozi walioweza kuwa washindi kakati chama hicho ni kama wafuatao:
Benjamin Mkapa
na
Jakaya Mrisho Kikwete
. Hawa ndio viongozi waliongoza nchi kipindi cha miaka ishirini.
Katika historia ya CCM kumekuwa na wenyeviti watano:
Viungo vya nje
|
---|
Mwenyekiti wa Taifa
| |
---|
Makamu Mwenyekiti (bara)
| |
---|
Makamu Mwenyekiti (Zanzibar)
| |
---|
Katibu Mkuu
| |
---|
Katibu Muundo
| |
---|
Katibu Uenezi
| |
---|
Katibu Masuala ya siasa na mahusiano ya kimataifa
| |
---|
Katibu Uchumi
| |
---|
Mengineyo
| |
---|