Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bizanti
(pia
Byzantium
au
Byzantion
kutoka kwa
Kigiriki
Βυζ?ντιον
) ilikuwa
mji
wa
Ugiriki ya Kale
. Wakati wa
Dola la Roma
jina lake lilibadilishwa kuwa
Konstantinopoli
na tangu
karne ya 20
inajulikana kama
Istanbul
.
Jina la Kigiriki
Byzantion
liliendelea kutumika kama jina badala ya Konstantinopoli mara kwa mara na kuwa chanzo cha "
Ufalme wa Bizanti"
jinsi sehemu ya
mashariki
ya Dola la Roma ilivyoitwa baada ya mwisho wa
utawala
wa
Kiroma
katika
magharibi
.
[1]
[2]
Mji wa Bizanti uliundwa na
Wagiriki
kutoka
Megara
katika
karne ya 7 KK
ukaendelea kuwa mji wenye
lugha
ya Kigiriki hadi
uvamizi
wake na
Milki ya Osmani
mnamo
1453 BK
.
[3]
Mji uliundwa kwenye
rasi
iliyopo baina ya
Bahari ya Marmara
na mkono wa bahari inayojulikana kama "
Pembe ya Dhahabu
" hivyo inazungukwa na
maji
kwa pande tatu iliyosaidia kutetea mji.
Hakuna uhakika kuhusu vyanzo vya Bizanti. Kufuatana na kisa kimoja mji ulianziswa na Byzas, mwana wa mfalme wa Megara iliyokuwepo karibu na
Athene
.
Herodoti
alitaja mwaka
667 KK
kama mwaka wa kuundwa kwa mji, hivyo miaka 17 baada ya mji wa
Kalsedonia
uliopo upande mwingine wa
mlangobahari
wa
Bosporus
.
[4]
Bizanti ilikuwa hasa mji wa
biashara
kutokana na mahali pake kwenye lango pekee la
Bahari Nyeusi
. Bizanti baadaye ilivamia Kalsedonia iliyopo kuvukia Bosporus upande wa
Asia
iliyoendelea kama sehemu ya Bizanti.
Katika
karne ya 4
BK, wakati ilipokuwa sehemu ya Dola la Roma, Bizanti iliteuliwa na
Kaizari Konstantino I
kama
mji wake mkuu
ikajulikana pia kama "Nova Roma" (Roma Mpya) akiipamba na
majengo
mengi mazuri. Baadaye jiji hilo liliitwa Konstantinopoli (Kigiriki Κωνσταντινο?πολι?,
Konstantinoupolis
, yaani "mji wa Konstantino").