Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Batman
(
kifupi
cha Milima ya Batı Raman) ni
jina
la
mji mkuu
wa
Mkoa wa Batman
, katika
Uturuki
.
Mji
huo pia unajulikana kwa jina la
Kikurdi
Elih
au
Iluh
.
[1]
Ni mji ulioko katika
Mto Batman
ambao unajulikana sana kwa jina la Kikurdi kusini-mashariki mwa nchi ya Uturuki.
[2]
Mkoa wa Batman ni eneo muhimu kabisa la uzalishaji wa mafuta, na mji wa Batman una maeneo ya kale ya vifaa vya kale vya kuchimbia mafuta, ambavyo vilianzishwa tangu mwaka wa
1955
.
Kuna takriban
km
494 (mi 307) za bomba la kupitishia mafuta kutoka mjini Batman kuelekea
?skenderun
. Kuna njia ya reli iliyo karibu kidogo na Kurtalan ambayo imeunganisha njia hiyo hadi kutoka katika mji wa
Istanbul
. Katika mji wa Batman, pia kuna uwanja wa ndege wa mkoa.
Hadi kufikia
miaka ya 1950
, Batman ilikuwa kijiji kidogo, ila makampuni ya mafuta yalipoingia uchumi wa mji huo ukaanza kukua, na idadi ya makazi ya watu ikaanza kuongezeka.
Wafanyakazi wengi na ofisi nyingi za serikali zipo mjini. Kwa sasa idadi ya watu wasio na kazi katika mji huo inaanza kuonekana kuwa kubwa kuliko hapo awali.
|
---|
| |