Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bahari ya Baltiki
ni
bahari ya kando
ya
Atlantiki
katika
Ulaya ya Kaskazini
. Imezungukwa na nchi kavu pande zote isipokuwa kati ya
Denmark
na
Uswidi
kuna
mlangobahari
mwembamba wa kuiunganisha na
Bahari ya Kaskazini
.
Bahari ya Baltiki imepakana na nchi za
Uswidi
,
Ufini
,
Urusi
,
Estonia
,
Latvia
,
Lituanya
,
Poland
,
Ujerumani
na
Denmark
.
Sehemu ya
kaskazini
kabisa iko mpakani mwa Uswidi na Ufini katika
Ghuba ya Botnia
, sehemu ya
mashariki
kabisa katika
Ghuba ya Ufini
kwenye
mji
wa
Sankt Petersburg
. Sehemu ya
kusini
iko kwenye mpaka wa Poland na Ujerumani na sehemu ya
magharibi
kwa mji wa
Flensburg
karibu na mpaka wa Ujerumani na Denmark.
Njia ya kuunganisha Baltiki na Bahari ya Kaskazini ni milangobahari ya
Kattegat
na
Skagerak
. Mwanzoni wa Kattegat njia inapita kwenye
visiwa
vya Denmark na kuigawa katika njia
tatu
ndogo zinazoitwa
Oresund
, Belt Kubwa (
Kidenmark
:
Storebælt
) na Belt Ndogo (Kidenmark:
Lillebælt
).
Kijiografia
Baltiki ni mabaki ya
Enzi ya Barafu
iliyopita. Takriban miaka 12,000 iliyopita
Ulaya
yote ya Kaskazini ilifunikwa na ganda la
barafu
lenye
unene
wa
mita
mia
kadhaa. Wakati wa kupungua kwa
baridi
barafu ilianza kuyeyuka na kusababisha kutokea kwa
ziwa
kubwa sana ambalo ni mwanzo wa Baltiki. Ziwa hili lilipata njia ya kujiunga na
bahari
na kiasi cha
maji ya chumvi
yaliingia ndani. Hivyo
maji
ya Baltiki ni mchanganyiko wa maji ya chumvi na maji matamu. Kiasi cha
chumvi
ndani ya maji yake ni kidogo kulingana na maji ya bahari ya kawaida.
Kiasi cha chumvi ni kikubwa zaidi kwenye
kina
kuliko kwenye maji ya juu. Wakati maji yenye chumvi kidogo inatoka kwenye Kattegat kuelekea Bahari ya Kaskazini kuna pia mwendo wa maji ya chumvi chini yake ya kuingia katika Baltiki. Maji ya chumvi ni mazito kuliko maji matamu, hivyo yanakaa kwenye vilindi vya bahari na kuwa na mwendo wa kuingia ilhali wakati huohuo maji ambayo ni matamu zaidi yanapita juu yake kutoka Baltiki.
Mito
mikubwa inaingia katika Baltiki na kusababisha mwendo wa maji ya kutoka katika Kattegat na kuingia Atlantiki. Baadhi ya mito hiyo ni:
Oder
,
Vistula
,
Neman
,
Daugava
na
Neva
.
Miji mikubwa kando ya Baltiki ni:
- Stockholm
(Uswidi) 774,411 (pamoja na mitaa ya nje 1,729,274)
- Malmo
(Uswidi) 259,579
- Helsinki
(Ufini) 559,716 (pamoja na mitaa ya nje 1,200,000)
- Turku
(Ufini) 175,000
- Sankt Petersburg
(Urusi) 4,700,000
- Kaliningrad
(Urusi) 400,000
- Riga
(Latvia) 760,000
- Tallinn
(Estonia) 401,774
- Klaip?da
(Lituanya) 194,400
- Gda?sk
(Poland) 462,700 (
pamoja na mitaa ya nje
1,041,000)
- Szczecin
(Poland) 413,600
- Gdynia
(Poland) 255,600
- Kiel
(Ujerumani) 250,000
- Lubeck
(Ujerumani) 216,100
- Rostock
(Ujerumani) 212,700
- Copenhagen
(Denmark) 502,204 (pamoja na mitaa ya nje 1,823,109)
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Ulaya
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Bahari ya Baltiki
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|