Antoku ( 22 Desemba , 1178 – 25 Aprili , 1185 ) alikuwa mfalme mkuu wa 81 ( Tenno ) wa Japani . Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Tokohito , na alikuwa mwana wa Tenno Takakura . Mwaka wa 1180 alimfuata babake. Ingawa mdogo wake, Go-Toba , alitangazwa kumfuata mwaka wa 1183, Antoku akachukuliwa na kukimbia mji mkuu, yaani kulikuwa na wafalme wawili hadi kifo chake Antoku.