Sir Andre Konstantin Geim (amezaliwa 21 Oktoba , 1958 ) ni mwanafizikia kutoka nchi ya Urusi aliyeshika uraia wa Uingereza na Uholanzi . Hasa amechunguza grafini . Mwaka wa 2010 , pamoja na Konstantin Novoselov , alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia . Mwaka wa 2012 alipewa cheo cha "Sir" cha Uingereza.