Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ananda
(
karne ya 5
?
4 KK
) alikuwa mhudumu mkuu wa
Buddha
na mmoja wa wanafunzi wake wakuu kumi. Miongoni mwa wanafunzi wengi wa Buddha, Ananda anaheshimiwa hasa kwa kuwa na
kumbukumbu
bora zaidi. Hivyo mafundisho mengi ya Buddha ambayo yamehifadhiwa katika
maandiko
ya
Sutta-Pi?aka
(
P?li
; Sanskrit Sutra-Pitaka) yanategemea kukumbuka kwake. Kwa sababu hiyo, anaheshimiwa kama
Mweka Hazina wa Dhamma
, wakati
Dhamma
(
Kisanskrit
: dharma) inamaanisha mafundisho ya Buddha.
Sehemu ya
mapokeo
inasema kwamba Ananda alikuwa
binamu
wa Buddha. Alitawazwa kuwa
mtawa
na Pu??a Mant?n?putta akawa
mwalimu
wake. Baadaye Buddha alimchagua kuwa mhudumu wake.
Aliandamana na Buddha kwa
maisha
yake yote, akitenda sio tu kama msaidizi, bali pia
katibu
na msemaji wake.
?nanda ni mmoja wa watu wanaopendwa sana katika
Ubuddha
. Alijulikana kwa kumbukumbu yake,
elimu
na
huruma
, na mara nyingi alisifiwa na Buddha kwa mambo haya.