Alberto Mkuu alivyochorwa na
Tommaso da Modena
mwaka
1352
Alberto Mkuu
(
Lauingen
,
Donau
, leo nchini
Ujerumani
,
1205
hivi -
Cologne
, Ujerumani,
15 Novemba
1280
) ni jina alilopewa kwa heshima
askofu
Alberto wa Bollstadt (au wa Cologne) kutokana na mchango wake mkubwa upande wa
elimu
ya kawaida na ile ya
dini
na vilevile upande wa
uchungaji
na wa upatanishi wa watu na watawala.
Mtawa huyo wa
Shirika la Wahubiri
anahesabiwa kuwa
mwanafalsafa
na
mwanateolojia
bora wa
Ujerumani
katika
Karne za Kati
.
Alijitahidi kulinganisha
imani
na
akili
akiingiza
falsafa
ya
Aristotle
katika
Ukristo
, jambo lililoendelezwa na mwanafunzi wake bora,
Thoma wa Akwino
.
Alitangazwa na
Papa Gregori XV
kuwa
mwenye heri
mwaka
1622
, na baadaye alitangazwa na
Papa Pius XI
kuwa
mtakatifu
na
mwalimu wa Kanisa
tarehe
16 Desemba
1931
.
Mwaka
1941
Papa Pius XII
alimtangaza
msimamizi
wa
wanasayansi
.
Sikukuu
yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe
15 Novemba
[1]
.
De animalibus
Alberto, mtoto mdogo wa mtawala wa Bollstadt, alizaliwa Lauingen (
Svevia
, Ujerumani) lakini mwaka haujulikani:
1205
,
1206
kama si
1193
.
Vilevile hakuna hakika kuhusu elimu yake ya msingi, kama aliipata nyumbani au shuleni, lakini ujanani alitumwa kwenye
chuo kikuu
cha
Padova
(
Italia
), maarufu kwa masomo yaliyompendeza zaidi:
lugha
,
hoja
,
hisabati
,
falaki
na
muziki
.
Akiwa huko, alikuwa anahudhuria
ibada
katika kanisa la Wadominiko, ambao
utakatifu
wa maisha yao ulichangia, pamoja na uhusiano wake wa dhati na
Mungu
, kumfanya atamani kuwa mmojawao hata akaweza kushinda upinzani wa
familia
yake.
Mwaka
1223
, baada ya kusikia hotuba ya
Jordano wa Saksonia
,
mwalimu mkuu
wa pili katika historia ya
Shirika la Wahubiri
, alijiunga na utawa huo ulioanzishwa na
Dominiko Guzman
. Jordano mwenyewe alimvika
kanzu
ya shirika.
Alipomaliza masomo yake, ama Padova ama kwingine, na kupata
upadrisho
, alitumwa kufundisha katika vituo vya
teolojia
vilivyounganika na
konventi
za shirika huko
Hildesheim
,
Freiburg in Brisgau
,
Regensburg
,
Strasburg
na
Cologne
mmoja kati ya miji mikuu ya mikoa, ambapo aliishi kwa awamu kadhaa na hatimaye ukawa mji wake.
Akiwa katika
konventi
ya mji huo, akisoma
Liber Sententiarum
ya
Petro Lombardo
mwaka
1245
, aliagizwa kwenda
Paris
(
Ufaransa
) alipojipatia
digrii
katika kituo kikuu cha huko, maarufu kuliko vyote upande wa teolojia.
Tangu hapo alianza kazi yake kubwa ya kuandika, mbali ya kutekeleza ma
jukumu
makubwa alivyozidi kupewa.
Akiwa safarini alisikilizwa na
Thoma wa Akwino
, kijana mkimya mwenye kutafakari, ambaye Alberto alitambua ukuu wa akili yake akamtabiri umaarufu wa kimataifa. Kati yao kukawa na
heshima
na
urafiki
mkubwa hadi mwisho. Huyo mwanafunzi mpya aliongozana naye hadi Paris halafu (
1248
) Cologne, ambapo Alberto alikuwa amechaguliwa kuwa
gombera
wa kwanza, wakati Thoma akawa mwalimu wa pili na
Magister Studentium
("mwalimu wa wanafunzi").
Katika
mkutano mkuu
wa Wadominiko uliofanyika
Valenciennes
mwaka
1250
, pamoja na Thoma na
Petro wa Tarentaise
, alitunga taratibu za masomo na za stahili shirikani.
Mwaka
1254
alichaguliwa
mkuu wa kanda
ya
Ujerumani
, wadhifa mgumu alioshughulikia vizuri sana. Alijitokeza kwa
ari
yake katika kutembelea
jumuia
za eneo lake kubwa, lililojumlisha
Ulaya Kaskazini
na
ya Kati
, huku akihimiza
uaminifu
kwa mafundisho na mifano ya Mt. Dominiko.
Mwaka
1256
alikwenda
Roma
ili kutetea
mashirika ya ombaomba
dhidi ya mashambulizi ya
Wiliamu wa Saint-Amour
, ambaye kitabu chake
De novissimis temporum periculis
hatimaye kililaaniwa na
Papa Aleksanda IV
tarehe
5 Oktoba
1256.
Akiwa Roma,
vipawa
vyake viligunduliwa na
Papa
aliyetaka awe naye ili kufaidika na mashauri yake ya kiteolojia. Hivyo Alberto alishika nafasi ya
mwalimu wa nyumba ya Papa
na kufafanua
Injili ya Yohane
.
Mwaka
1257
alijiuzulu kama mkuu wa kanda ili ajitose kusoma na kufundisha.
Mwaka
1260
kwa uamuzi wa Papa huyohuyo, alipewa
daraja takatifu
ya
uaskofu
kwa ajili ya
Jimbo la Regensburg
, ambalo lilikuwa kubwa na maarufu, lakini wakati huo lilipitia matatizo mbalimbali. Basi, aliliongoza kwa
bidii
isiyokoma, akifaulu kurudisha
amani
mjini, kupanga upya
parokia
na nyumba za kitawa pamoja na kuchochea upya
huduma
za
huruma
.
Mwaka
1262
alijiuzulu, halafu miaka
1263
-
1264
alihubiri katika Ujerumani na
Ucheki
wa leo kwa agizo la
Papa Urban IV
akarudia kazi ya kufundisha na kuandika huko Cologne.
Kama mtu wa
sala
,
elimu
na
upendo
, aliingilia kwa mafanikio matukio mbalimbali ya
Kanisa
na
jamii
: hasa alipatanisha watu wa Cologne na
askofu mkuu
wao aliyekuwa ameharibu sana.
Mwaka
1270
alimuandikia Thoma, aliyekuwa Paris, ili kumsaidia dhidi ya hoja za
Sigieri wa Brabante
na wafuasi wa
Averroe
. Ilikuwa kitabu cha pili dhidi ya huyo
mwanafalsafa
Mwarabu
(cha kwanza kiliandikwa mwaka 1256 kwa jina
De Unitate Intellectus Contra Averroem
).
Mwaka
1274
aliitwa na
Papa Gregori X
ashiriki
Mtaguso wa pili wa Lyon
, ambamo alifanya kazi kubwa ili kurudisha
umoja
kati ya
Kanisa la Kilatini
na
lile la Kigiriki
. Huko alipata taarifa ya kifo cha Thoma akasema, "Mwanga wa Kanisa umezimika".
Alijitokeza tena kwa nguvu mwaka
1277
, ilipotangazwa nia ya
Etienne Templier
,
askofu mkuu
wa Paris pamoja na wengine ya kulaani maandishi ya Thoma kama yenye
uzushi
. Ili kumtetea alifunga safari kwenda Paris kuyafafanua.
Mwaka
1278
(alipoandika
wasia
wake) alianza kusahausahau mambo, na mwili wake uliodhoofishwa na maisha magumu ya kujinyima na ya kazi ulizidi kushindwa na uzee hadi akafa tarehe 15 Novemba 1280 katika
chumba
chake konventini.
Alizikwa katika
kanisa
la
parokia
ya
Mt. Andrea
ya Cologne.
Vitabu vyake vingi vinahusu
fani
zote za elimu ya wakati ule:
mantiki
,
sayansi
mbalimbali,
elimunafsia
,
falsafa
,
maadili
,
siasa
,
teolojia
, ufafanuzi wa
Biblia
n.k. Orodha yake inashangaza kwa upana wa
mada
alizozikabili kitaalamu. Ndiyo sababu
Papa Pius XII
alimpangia jina la “Doctor universalis” (yaani Mwalimu wa kila jambo).
Akiwa
mtaalamu
mkuu wa
biolojia
wakati wake, aliunganisha vizuri sayansi na
ufunuo
wa Mungu, falsafa na teolojia. Ulinganifu huo unamfanya awe karibu na watu wa leo katika maswali wanayojiuliza kuhusu asili na maendeleo ya
ulimwengu
.
Upana wa mawazo yake ulijitokeza hasa katika kuelekeza Kanisa lipokee falsafa ya
Aristotle
katika
ufafanuzi
wa
ulimwengu
, kutokana na hakika ya kwamba kila kinachokubaliwa na
akili
nyofu kinapatana na
imani
katika
ufunuo
wa Mungu. Kwa namna hiyo Alberto aliwezesha falsafa kuwa fani inayojitegemea, ikishirikiana na kuunganika na
teolojia
katika umoja wa
ukweli
tu, bila kuchanganyikana.
Yeye alifaulu kushirikisha hata mawazo hayo kwa namna sahili na ya kueleweka, kama alivyofanya katika mahubiri aliyowapa watu wa kila kiwango cha elimu, waliovutiwa na maneno yake na mfano bora wa maisha yake.
- Attwater, Donald and Catherine Rachel John.
The Penguin Dictionary of Saints
. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993.
ISBN 0-14-051312-4
.
- Collins, David J. "Albertus, Magnus or Magus?: Magic, Natural Philosophy, and Religious Reform in the Late Middle Ages."
Renaissance Quarterly
63, no. 1 (2010): 1?44.
- Wallace, William A. (1970).
"Albertus Magnus, Saint"
. In Gillispie, Charles.
Dictionary of Scientific Biography
.
1
. New York: Scribner & American Council of Learned Societies. pp. 99?103.
ISBN
9780684101149
.
http://www.u.arizona.edu/~aversa/scholastic/Dictionary%20of%20Scientific%20Biography/Albertus%20Magnus%20(Wallace).pdf
.
Archived
8 Machi 2021 at the
Wayback Machine
.
WikiMedia Commons