Mtakatifu
ni
binadamu
aliye hai au aliyekufa ambaye
dini
fulani au watu mbalimbali wanamheshimu kwa namna ya pekee kwa jinsi alivyoonekana kuwa karibu zaidi na
Mungu
hata akashirikishwa
utakatifu
wake. Kwa hiyo hutazamwa kama kielelezo cha
uadilifu
na pengine kama
mwombezi
pia.
Jina
linalotumiwa zaidi na
Wayahudi
ni
tzadik
(mtu wa
haki
, mwadilifu), aliyejitahidi kufuata
Torati
.
Kitabu
cha
Talmud
kinasema kila mara
duniani
walau watu 36 wa namna hiyo (
tzadikim
) wanaishi kati yetu na kuzuia
ulimwengu
usiangamizwe kama
adhabu
ya
dhambi
.
Pengine wanaitwa hivyo hata watu wa
mataifa
, hasa waliojitahidi kusaidia Wayahudi, k.mf. wakati wa
dhuluma
. Baadhi yao wanaorodheshwa na kupewa
heshima
rasmi.
Mwanzoni mwa
Kanisa
kila
Mkristo
aliitwa mtakatifu kwa sababu alitengwa na ulimwengu na kuwekwa
wakfu
kwa Mungu aliye mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu.
Sifa hiyohiyo ilitolewa pia kwa
mahali
,
siku
, vitu n.k. kutokana na matumizi yake ya kidini.
Kwa
Wakatoliki
mtakatifu
ni yule aliyemfuata
Yesu Kristo
, akiishi kwa
upendo
na
maadili
mengine yanayoutegemea, hasa aliyeyatekeleza kwa kiwango cha
ushujaa
katika
kufia dini
, kutoa
uhai
wake katika kuhudumia wengine au katika
maisha
ya kila siku.
Utakatifu si wa aina moja, bali kila binadamu anatakiwa kuitikia siku kwa siku
wito
maalumu aliopewa na Mungu. Hivyo yeyote anaweza na kupaswa kulenga utakatifu, bila kujali sifa zake za
kimaumbile
tu.
Ili kuzuia
udanganyifu
, tangu mwanzoni mwa
milenia
ya pili
Kanisa Katoliki
linamuachia
Papa
kusimamia
kesi
ndefu za kumtangaza mtakatifu mpya, miaka baada ya
kifo
chake.
Wakatoliki wanawapatia
Bikira Maria
na watakatifu wengine heshima ya pekee kama
marafiki
wa Mungu, lakini si
ibada
halisi ambayo ni kwa Mungu tu. Heshima hiyo inadai waumini wajitahidi pia kufuata mifano yao kama wao walivyofuata ile ya
Yesu
.
Katika Makanisa ya Kiorthodoksi
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Makanisa ya Kiorthodoksi
yanamuita mtakatifu hasa anayesadikiwa yuko katika
paradiso
, kuanzia
Abeli
,
Adamu
na
Eva
,
Musa
na
manabii
wengine, lakini pia
malaika
.
Ni Mungu anayefunua watakatifu wake kwa kuitikia
sala
anazotolewa kwa kuwapitia hao hata akatenda
miujiza
. Wakristo wanaanza kuwatambua lakini
uamuzi
wa mwisho unachukuliwa na
sinodi ya maaskofu
.
Waorthodoksi
na
Waorthodoksi wa Mashariki
wanawatendea watakatifu kama watu hai, kwa sababu wanaishi
mbinguni
pamoja na
Kristo mfufuka
, ingawa
miili
yao haijaungana tena na
roho
zao.
Kila mtu
anapobatizwa
anapewa jina la mtakatifu fulani kama
msimamizi
kwa maisha yake yote.
Madhehebu
mengi ya
Uprotestanti
hayakubali mawazo hayo, yakipenda kusisitiza kwamba
wokovu
unamtegemea Mungu tu. Hata hivyo mara nyingi waamini bora wanakumbukwa kwa heshima na kuchukuliwa kama mfano (taz.
Confessio augustana
art. 21).
Hasa
Waanglikana
wanakaribia msimamo wa Wakatoliki na kuadhimisha
sikukuu
za watakatifu kadiri ya
kalenda
maalumu.
Ingawa dini hiyo haikubali tofauti kati ya watu, Waislamu wengi wanapenda kuheshimu kwa namna ya pekee marafiki wa Mungu (
wali
), wakisadiki wana uwezo wa kutabiri, kuombea na kuponya.
|
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|