Mpeketoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Mpeketoni
Nchi Kenya
Kaunti Lamu
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 25 000
Barabara ya Mpeketoni

Mpeketoni ni mji wa Kenya katika kaunti ya Lamu [1] .

Si mji wa kale bali ulianzishwa katika miaka ya 1960 kama mradi wa kujenga makazi ya watu na rais wa jamhuri , Jomo Kenyatta .

Kwa asili eneo lilikaliwa na Wabajuni lakini wakati wa uhuru , na baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki , Wakenya wengi walirudi kutoka Tanzania hasa Wakikuyu , walio sehemu kubwa ya wakazi wa leo, pamoja na Waluo na Wakamba .

Mashamba yaliyoanzishwa na walowezi hao yanaendelea hadi leo. Kilimo ni hasa ya mahindi , pamba , muhogo , korosho , maembe , tikiti maji na ndizi .

Kabla ya ukoloni wa Kiingereza eneo lilikuwa chini ya usultani wa Zanzibar . Wafanyabiashara ya watumwa walitumia njia ya pwani kupeleka watumwa hadi Lamu . Hadi sasa mwembe mkubwa unakumbusha mahali ambako misafara ya watumwa ilipumzika na wafungwa walikula maembe na kuacha mbegu .

Karibu na Mpeketoni kuna ziwa Kenyatta .

Vijiji ndani ya tarafa ni pamoja na Kiongwe, Baharini, Mkunumbi, Bomani, Uziwa, Mapenya, Lakeside, Kibaoni.

Mashambulizi ya al-Shabaab 2014 [ hariri | hariri chanzo ]

Tarehe 16 Juni 2014 mji huo ulishambulia na kikosi cha al-Shabaab kutoka Somalia walioua watu 48. Mnamo saa 3 jioni waliingia katika mji kwa kutumia magari 3 wakati wakazi wengi walikuwa wakiangalia mechi ya Kombe la Dunia la FIFA . Washabaab walitangulia kushambulia kituo cha polisi lakini walishindwa kuingia kutokana na upinzani wa maafisa . Waliendelea kushambulia hoteli , mabaa, benki na ofisi za serikali ilhali walifyatulia risasi hovyo wananchi waliowaona pamoja na watoto wadogo na wakinamama. [2]

Baada ya saa sita usiku waliondoka tena lakini njiani waliua wananchi wengine, kwa mfano watu sita huko Kibaoni.

Tazama pia [ hariri | hariri chanzo ]

Tanbihi [ hariri | hariri chanzo ]

Viungo vya nje [ hariri | hariri chanzo ]

  • www.wimvandenburg.nl. shirika la Kiholanzi linalotoa misaada kwa miradi katika Mpeketoni