Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Melvin Schwartz
(
2 Novemba
1932
-
28 Agosti
2006
) alikuwa
mwanafizikia
Mmarekani. Mwaka
1988
alipokea
Tuzo ya Nobel
ya Fizikia
pamoja na
Leon Max Lederman
na
Jack Steinberger
kwa mafanikio yao ya kugundua mbinu za kushughulika ma
neutrino
ambazo ni chembe ndogo sana ya kinyuklia isiyo na chaji na haipasuliki.
Alikuwa mtoto wa mji wa New York akasoma
Bronx High School of Science
na
chuo kikuu
cha
Columbia University
alipokuwa mwanafunzi wa mshindi wa Tuzo Nobel
Isidor I. Rabi
na profesa msaidizi tangu 1958.
Mwaka
1966
alihamia
Chuo Kikuu cha Stanford
alipokuta mashine mpya ya kuharakisha mwendo wa chembe za kinyuklia iliyomsaidia kuendeleza utafiti wake.
Mwaka
1991
akawa mkurugenzi msaidizi wa idara ya fizikia ya kinyuklia kwenye taasisi ya
Brookhaven National Laboratory
(yaani Maabara ya Kitaifa kule Brookhaven, Marekani) alipowahi kutekeleza majaribio yake yaliyompatia tuzo ya Nobel baadaye. Wakati ule akawa pia profesa kamili huko Columbia.
Alistaafu mwaka 2000.
|
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Melvin Schwartz
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|