Archibald Campbell Mzolisa Jordan ( 30 Oktoba 1906 - 20 Oktoba 1968 ) alikuwa mwandishi na mwanahistoria wa Afrika Kusini . Hasa anajulikana kwa riwaya yake ya Kixhosa Ingqumbo Yeminyanya (= Hasira ya Mababu). Pia aliandika tahakiki za fasihi ya Kixhosa zilizotolewa baada ya kifo chake tu. Mwaka wa 1961 aliruhusiwa na serikali kuhama Afrika Kusini na akawa profesa ya Lugha na Fasihi za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Wisconsin , Marekani .