Dikteta
(kutoka
Lat.
dictator
yaani mwenye kutoa amri kama imla) ni neno la kumtaja mtawala asiyebanwa na sheria na kutumia nguvu ya dola kuendeleza utawala wake na kutokubali upinzani dhidi yake. Pale ambako mtu au kundi la watu hutawala kwa mbinu huu hali ya kisiasa huitwa
udikteta
.
Mfalme
anayeweza kuwa na madaraka yaleyale haitwi dikteta.
Asili ya cheo
hariri
Kiasili "dikteta" ilikuwa cheo cha muda kwa ajili ya afisa wa
jamhuri ya Roma
ya kale. Kwa kawaida Waroma wa Kale waligawa madaraka makuu kati ya maafisa watendaji wawili walioitwa
konsuli
.
Lakini katika hali ya hatari kuu kama vita au ghasia kubwa
senati
ya Roma -yaani bunge- iliweza kuamua kuwa na dikteta kwa muda. Uteuzi wa dikteta ulikuwa mkononi mwa makonsuli au kama konsuli mmoja alikuwa mbali na Roma pia mkononi mwakonsuli aliyekuwepo.
Muda wa ofisi ya dikteta ilikuwa hadi miezi 6 lakini mara nyingi dikteta alirudisha madaraka yake kwa senati mara baada ya kumaliza shughuli kama kushinda vita au kugandamiza ghasia.
Dikteta alikuwa mtendaji mkuu wa serikali na amiri mkuu wa jeshi. Alishika pia madaraka ya kihakimu. Aliweza kuwaondoa maafisa wote wengine madarakani, aliweza kutoa hukumu ya mauti na kuagiza kifo cha mtu yeyote. Baada ya kumaliza kipindi chake hakuweza kuwajibika au kushtakiwa kwa maazimio na matendo yake. Kwa kawaida madiketa wa Roma walishirikiana na senati lakini hawakupaswa kufanya hivyo.
Dikteta wa kisasa
hariri
Leo hii "dikteta" si cheo rasmi tena lakini namna ya kumtaja mtawala mkali anayeshika mamlaka yote mkononi mwake na kutawala kwa mabavu. Mara nyingi dikteta hakubali uchaguzi wa kisiasa au anahakikisha uchaguzi si huru. Haheshimu haki za kibinadamu kama zinamsumbua. Anatoa amri kama sheria; kama anaruhusu kuwepo kwa bunge na mawaziri ni sharti wafuate maagizo yake. Hakubali upinzani dhidi yake na matamko ya mawazo yasiyopendezwa naye.
Katika
karne ya 20
madikteta mara nyingi walitumia
mfumo wa chama kimoja
cha kisiasa, usimamizi wa magazeti, redio na televisheni.
Kuna madikteta waliofika madarakani kwa njia ya uchaguzi lakini baadaye waliondoa upinzani na kuzuia uchaguzi huru. Mfano wake alikuwa
Adolf Hitler
wa
Ujerumani
; chama chake cha
NSDAP
kilipata kura nyingi kidogo katika uchaguzi wa Januari 1933 akaanzisha serikali kwa msaada wa chama kidogo akatumia mamlaka yake juu ya polisi kwa kuwakamata wapinzani wengi na kutisha mahakama pamoja na wabunge wa upinzani kwa hiyo alipewa madaraka ya kidikteta na bunge; baada ya kuwa na madaraka haya alipiga vyama vingine marufuku akatawala peke yake.
Kuna madikteta waliofika madarakani kwa njia ya
mapinduzi ya kijeshi
; mifano yake ni
Francisco Franco
wa
Hispania
au
Idi Amin
wa
Uganda
. Wote walikuwa maafisa wa jeshi walitumia mamlaka yao juu ya wanajeshi kupindua serikali halali kwa njia ya mabavu na kujifanyia wenyewe watawala. Mara nyingi hao madikteta wa kijeshi huanza kwa vyeo kama mwenyekiti wa kamati ya kijeshi au mwakilishi mkuu wa wanajeshi lakini baada ya muda mfupi hakuna tena anayeweza kuwapinga.
Kuna madikteta wengine wanaopanda ngazi ndani ya udikteta wa kikundi au chama ambako awali kamati ilitawala kwa pamoja. Mfano ni
Josef Stalin
wa Urusi (
Umoja wa Kisovyeti
) alikuwa mwanzoni Katibu Mkuu wa
chama cha kikomunisti
tu na wala mkuu wa dola wala mkuu wa serikali. Alitumia nafasi yake kuondoa kwanza upinzani dhidi yake ndani ya chama na baada ya mabadiliko katika vyeo vya dola pia kuimarisha usimamizi wake wa maazimio wa vyama kuhusu maafisa wa dola. Mwishowe alishtaki wapinzani wake kuwa wasaliti na kushawishi mahakama ya kuwahukumu. Tangu miaka 1935-36 hakuwa tena na mpinzani na matakwa yake yalikuwa kama sheria.
Madikteta kadhaa wa karne ya 20
hariri
- Benito Mussolini
,
Italia
- Josef Stalin
,
Soviet Union
- Adolf Hitler
,
Ujerumani
- Francisco Franco
,
Hispania
- Chiang Kai-shek
,
China
, baadaye
Taiwan
- Mao Zedong
,
China
- Fidel Castro
,
Kuba
- Augusto Pinochet
,
Chile
- Idi Amin
,
Uganda
- Sani Abacha
,
Nigeria
- Mobutu Sese Seko
,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
- Pol Pot
,
Kambodia
- Saddam Hussein
,
Iraq