Chekoslovakia
ilikuwa nchi ya
Ulaya
kati ya
1918
na
1992
iliyounganisha nchi za leo za
Ucheki
na
Slovakia
.
Tangu
1 Januari
1993
Chekoslovakia imegawiwa kwa amani kuwa nchi mbili za
Jamhuri ya Kicheki
na
Jamhuri ya Slovakia
.
Chekoslovakia ilianzishwa 1918 baada ya kuporomoka kwa
Austria-Hungaria
wakati wa mwisho wa
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia
. Iliunganisha majimbo
Bohemia
na
Moravia
yaliyokaliwa na Wacheki upande wa
Austria
na maeneo ya
Hungaria
yaliyokaliwa na Waslovakia.
Chekoslovakia ilikuwa nchi ya mataifa na utamaduni mbalimbali. Mataifa makubwa yalikuwa Wacheki (51,5?% ), Wajerumani (23,4?%) na Waslovakia (14?%) pamoja na vikundi vikubwa kidigo vya Wahungaria, Waukraine, Waromani na Wapoland.
Mwaka
1938
dikteta
Adolf Hitler
wa
Ujerumani
alivamia sehemu za Ucheki. Slovakia ikawa nchi ya kujitegemea chini ya Ujerumani.
1945
baada ya
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
umoja wa Ucheki na Slovakia ukarudishwa chini ya usimamizi wa
Urusi
. Warusi walihakikisha ya kwamba
Chama cha Kikomunisti
kilipata serikali. Utawala wa kikomunisti ulidumu hadi
1989
. Baada ya kuanguka kwa
ukuta wa Berlin
utawala huu ulikwisha mwisho wa mwaka 1989.
Pande zote mbili za Ucheki na Slovakia ziliona ugumu wa kupatana. 1991 Umoja ulimalizwa na nchi mbili zilitoka katika shirikisho la Chekoslovakia.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Ulaya
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Chekoslovakia
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|