Kitabu cha Zaburi
ni kimojawapo kati ya
vitabu
vya
Tanakh
(yaani
Biblia ya Kiebrania
) na kwa hiyo pia vya
Agano la Kale
ambalo ni sehemu ya kwanza ya
Biblia ya Kikristo
.
Kama vitabu vingine vyote vya
Biblia
, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa
historia ya wokovu
ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya
ufunuo
wa
Mungu
kwa
binadamu
.
Kina
sura
150; kila sura ni
zaburi
moja. Zaburi ni aina ya
sala
iliyotungwa kama
shairi
au
wimbo
. Zaburi zinafundisha jinsi
binadamu
awezavyo kuzungumza na
Mwenyezi Mungu
.
Kwa hiyo kitabu cha Zaburi kinatumiwa na
Wayahudi
na
Wakristo
kama kitabu cha
sala
.
Mada
za zaburi hasa ni
sifa
za
Mungu
,
shukrani
, ma
ombolezo
,
huzuni
na
toba
,
furaha
na
imani
,
elimu
ya ki
dini
, na
ombi
la
ushindi
dhidi ya maadui wasiomcha Mungu.
Zaburi nyingi zimetungwa kama shairi la
Kiebrania
; mara nyingi fungu moja linarudia wazo la fungu lililopita, k.m. katika Zaburi 22, mistari 1-2:
- Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
- Mbona uko mbali sana kunisaidia, mbali na maneno ya kilio changu?
- Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu;
- napiga yowe usiku, lakini nafuu sipati.
Katika kitabu hicho zaburi kadhaa zimewekwa pamoja: kwa mfano, Zaburi za
Wakorahi
(baadhi zikiwa 42?49), za
Asafu
(73?83), za kumsifu Mungu aliye
Mfalme
au Mtawala wa wote (93?99) au Zaburi za
kuhiji
(120?134).
Baadaye Zaburi ziligawanywa katika vitabu vitano: 1?41; 42?72; 73?89; 90?106; 107?150. Kila kimojawapo kinamsifu Mungu katika mstari wake wa mwisho: 41:13; 72:19; 89:52; 106:48; na Zaburi yote ya 150. Inawezekana kuwa mgawanyo huo ulifanyika ili kuiga mgawanyo wa vitabu vitano vya kwanza vya Biblia, yaani
Torati
.
Baadhi ya Zaburi zinazojulikana sana ni:
Wewe, Mungu, Bwana wetu,
jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni.
Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao
umeiweka misingi ya nguvu;
kwa sababu yao wanaoshindana nawe;
uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi.
Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako,
mwezi na nyota ulizoziratibisha;
mtu ni kitu gani hata umkumbuke,
na binadamu hata umwangalie?
Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu;
umemvika taji ya utukufu na heshima;
umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
Kondoo, na ng’ombe wote pia;
naam, na wanyama wa kondeni;
ndege wa angani, na samaki wa baharini;
na kila kipitiacho njia za baharini.
Wewe, Mungu, Bwana wetu,
Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Nimekuinulia macho yangu, wewe uketiye mbinguni.
Kama vile macho ya watumishi kwa mkono wa bwana zao;
kama macho ya mjakazi kwa mkono wa bibi yake;
hivyo macho yetu humwelekea Bwana, Mungu wetu,
hata atakapoturehemu.
Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu sisi,
kwa maana tumeshiba dharau.
Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha,
na dharau ya wenye kiburi.
Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia;
Bwana, uisikie sauti yangu.
Masikio yako na yaisikilize sauti ya dua zangu.
Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu,
Ee Bwana, nani angesimama?
Lakini kwako kuna msamaha, ili Wewe uogopwe.
Nimemngoja Bwana, roho yangu imemngoja,
na neno lake nimelitumainia.
Nafsi yangu inamngoja Bwana,
kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,
naam, walinzi waingojavyo asubuhi.
Ee Israeli, umtarajie Bwana;
maana kwa Bwana kuna fadhili,
na kwake kuna ukombozi mwingi.
Yeye atawakomboa Israeli na maovu yake yote.
|
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Kitabu cha Zaburi
kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|