Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
|
|
|
|
Yuda Iskarioti
(kwa
Kiebrania
????? ?????????),
Myahudi
wa
karne ya 1
, alikuwa mmojawapo wa
Mitume wa Yesu
, maarufu kwa kuwa alimsaliti
mwalimu
wake apate vipande thelathini vya
fedha
(
Injili ya Mathayo
26:14-16).
Ni tofauti na
mtume
mwenzake
Yuda Tadei
.
Kwa
Kigiriki
, katika
Agano Jipya
anaitwa Ιουδα? Ισκαριωθ (Ioudas Iskarioth) na Ισκαριωτη? (Iskariotes).
Kwa kuwa Yuda ni jina la
babu
wa
kabila
kubwa la
Israeli
lililobaki baada ya yale ya
Kaskazini
kupotea
uhamishoni
(
722 KK
), lilitumiwa sana na
Wayahudi
, hata wawili kati ya mitume hao wanaitwa hivyo.
Ndiyo sababu ilibidi kuwatofautisha kwa jina la pili, ambalo kwake ni "Iskarioti", maana yake "mtu wa Kariot" (
Ish Kariot
) kutokana na
kijiji
cha asili (
Keriot-Chezron
kinachotajwa tu katika
Kitabu cha Yoshua
15:25, kikiwa
Kusini
kwa
Yudea
, mipakani kwa
Edomu
, kwenye
Neghev
.
Tafsiri
nyingine inategemea jina
Ekariot
("
gaidi
") walilopewa wapiganiauhuru wakali zaidi, waliokuwa tayari kuua wakoloni popote pale.
Tafsiri ya tatu inazingatia neno la
Kiaramu
sheqarya'
au
shiqrai
, linalomaanisha mtu
dhalimu
; "
tapeli
" linaweza kutafsriwa
ishqaraya
.
Tafsiri ya mwisho inategemea neno lingine la
lugha
hiyo,
sakar
, yaani
anayekabidhi
.
Yuda anatajwa katika
Injili
na mwanzoni mwa
Matendo ya Mitume
.
Humo tunasoma kwamba alikuwa
mwekahazina
wa kundi la Mitume (
Injili ya Yohane
12:6) mwenye
tabia
ya
udokozi
ambaye hatimaye alimuuza
Yesu Kristo
kwa ma
adui
wake wa
Baraza la Israeli
(
Injili ya Mathayo
26:47-49).
Mapema baada ya tukio hilo alikufa vibaya (
30
B.K.
) na nafasi yake ikashikwa na
Mtume Mathia
.
|
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Yuda Iskarioti
kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|