Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yordani
(kwa
Kiebrania
: ??? ?????
nehar hayarden
; kwa
Kiarabu
: ??? ??????
nahr al-urdun
) ni
mto
mdogo katika
Mashariki ya Kati
lakini ni kati ya mito inayojulikana sana
duniani
kwa sababu imetajwa mara nyingi katika
Biblia
.
Hivyo katika
dini
za
Uyahudi
na
Ukristo
Yordani ina maana ya pekee: kwa
Wayahudi
unakumbusha tukio la
Yoshua
kuwaongoza
babu
zao kuuvusha pakavu wakati wa kuvamia nchi ya
Kanaani
. Kwa Wakristo unakumbusha pia
ubatizo wa Yesu
kwa
mikono
ya
Yohane Mbatizaji
.
Kwa sehemu kubwa ya njia yake uko chini ya
usawa wa bahari
na ni mpaka kati ya
ufalme
wa
Yordani
upande wa
mashariki
na maeneo ya
Palestina
na
Israel
upande wa
magharibi
.
Chanzo
cha Yordani ni mito minne inayobubujika karibu na
mlima Hermoni
mpakani kwa Israel,
Lebanon
na
Syria
.
Mito ya chanzo inaungana katika Israel ya kaskazini.
Yordani hupita eneo la
Galilaya
inapounda
ziwa Genesareti
na baada ya kutoka hapo inatelemka kwa kupindapinda mara nyingi hadi
Bahari ya Chumvi
.
Mdomo
wake uko m 400 chini ya
usawa wa bahari
, hivyo Yordani ni mto wa pekee kabisa duniani.
Kiasi cha
maji
kwenye sehemu ya
kusini
ya mto kimepungua sana kwa sababu Israel inavuta sehemu kubwa ya maji kwa ajili ya matumizi ya
binadamu
katika
miji
yake.
Bonde la Yordani
ni sehemu ya
kaskazini
ya
Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki
linaloendelea katika
bonde la Araba
na kupita
Bahari ya Shamu
hadi kuonekana tena
Eritrea
.