Kuhariri Yohane wa Msalaba
Yohane wa Msalaba
(
Fontiveros
,
Castilia
,
Hispania
,
24 Juni
1542
-
Ubeda
, Hispania,
14 Desemba
1591
) ni jina la kitawa la
Juan de Yepes Alvarez
,
padri
wa
Kanisa Katoliki
na
mwanzilishi
(pamoja na
Teresa wa Yesu
) wa
urekebisho
wa shirika la
Wakarmeli
maarufu kama
Wakarmeli Peku
.
Anaheshimiwa kama
mtakatifu
na
mwalimu wa Kanisa
.
Sikukuu
yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe
14 Desemba
[1]
.
Yohane alizaliwa
Fontiveros
,
kijiji
cha
mkoa
wa
Castilia
(
Hispania
), tarehe
24 Juni
1542
akafariki
Ubeda
tarehe
14 Desemba
1591
.
Baba
yake,
Gonzalo de Yepes
, wa
ukoo
maarufu wa
Toledo
wenye asili ya
Kiyahudi
, alifukuzwa na
familia
yake na kunyimwa
urithi
kwa sababu ya
kumuoa
mfumaji
fukara
,
Catalina Alvarez
. Hivyo
hali
yao ilikuwa ngumu sana
kiuchumi
.
Tangu
utotoni
Yohane alielekea
huruma
kwa
maskini
na hasa
sala
.
Kati ya
1551
na
1559
alipata
elimu
na
ufundi
huko
Medina del Campo
(
kituo
cha
biashara
na masomo karibu na
Valladolid
), ambapo familia yake ilikuwa imehamia kufuatana na kifo cha baba yake.
Baadaye akawa
seremala
,
mshonaji
,
mchoraji
,
mchongaji
,
nesi msaidizi
na
mtumishi wa altare
, kufuatana na
vipawa
vyake na
maendeleo
yake katika masomo.
Akiwa na miaka 18 aliingia
shule
mpya ya
bweni
iliyoanzishwa na
Wajesuiti
huko Medina del Campo akasoma
lugha
na mengineyo kwa miaka mitatu. Alipomaliza alikuwa na
hakika
kuhusu
wito
wake wa kitawa.
Mwaka
1563
alijiunga na shirika la
Wakarmeli
, wakati
maisha ya jumuia
yalipokuwa yamelegea sana, na
wakati wa joto
wa mwaka huo alianza
unovisi
hukohuko Medina del Campo akichukua jina la Yohane wa
Mt. Matia
.
Kati ya
1564
na
1567
akasoma lugha na
falsafa
katika
chuo kikuu
maarufu cha
Salamanca
.
Mwaka
1567
alipata
upadirisho
akarudi Medina del Campo kuadhimisha
Misa ya shukrani
kati ya wanafamilia.
Huko akakutana na
Teresa wa Yesu
, ambaye alimfanya amuunge mkono katika kurekebisha shirika hilo lirudi kwenye
juhudi
za awali “kwa
utukufu
mkubwa zaidi wa
Mungu
”. Upande wake Teresa alianza kumheshimu sana akamuita "baba wa roho" yake, ingawa alimtania pia kutokana na
silika
yake ngumu na makini.
Kwa miezi kadhaa walishirikishana mawazo na malengo kwa ajili ya kuanza
urekebisho
mapema iwezekanavyo.
Tarehe
9 Agosti
1568
, alikwenda
Valladolid
ilipoanzishwa
monasteri
ya kwanza ya
Masista Wakarmeli Peku
akabaki huko hadi Oktoba ili kujifunza maisha ya urekebisho, halafu akaenda
Duruelo
(
Segovia
), akageuza nyumba ya wakulima kuwa
konventi
ya kwanza ya
Wakarmeli Peku
wanaume
(
28 Desemba
).
Mwanzoni walikuwa wanne. Waliporudia
nadhiri
zao kadiri ya
kanuni
asili ya shirika, kila mmoja alijichagulia jina jipya, naye akajiita “Yohane wa Msalaba”.
Mwishoni mwa mwaka
1572
, kwa ombi la Teresa, akawa
muungamishi
na makamu wa monasteri ya
Umwilisho
mjini Avila iliyongozwa na Teresa mwenyewe.
Ilifuata miaka ya
urafiki wa kiroho
na
ushirikiano
mkubwa kwa
faida
ya wote wawili. Ndipo vitabu bora vya Teresa na vile vya kwanza vya Yohane vilipoandikwa.
Kati ya mateso ya kimwili na ya kiroho yaliyompata kwa kupigania urekebisho, mbali ya kufukuzwa
konventini
, mojawapo ni lile la kufungwa miezi minane kwa
tuhuma
ya
uongo
katika
gereza
la shirika la
Toledo
(kuanzia tarehe
2 Desemba
1577
hadi alipotoroka
usiku
wa kuamkia tarehe
17 Agosti
1578
). Humo alinyanyaswa kwa namna mbalimbali.
Hata hivyo humohumo aliangaziwa na Mungu kutunga baadhi ya mashairi yake bora, yaliyompatia nafasi kati wa washairi mashuhuri wa
lugha
ya
Kihispania
.
Kisha kujisalimisha katika nyumba ya Wakarmeli Peku ya Toledo, Teresa na wenzake walishangilia sana
uhuru
wake. Baada ya
muda
mfupi wa
pumziko
kwa ajili ya kupata tena
nguvu
, alipangiwa kwenda katika
mkoa
wa
Andalusia
, alipoishi miaka 10 katika konventi mbalimbali, hasa
Granada
.
Alizidi kupewa vyeo muhimu shirikani hata kuwa makamu wa
mkuu wa kanda
, pia alikamilisha maandishi yake ya kiroho.
Halafu akarudi katika mkoa wake asili kama mmoja wa
halmashauri kuu
ya shirika la Teresa ambalo lilikuwa limeshapata uhuru kamili kisheria. Aliishi katika
Karmeli
ya
Segovia
kama mkuu wa
jumuia
.
Miaka ya mwisho ya maisha yake alijikuta ameachwa na wafuasi wake walio wengi.
Mateso hayo yote yalimfundisha kuvumbua
fumbo
la
msalaba
na kusonga mbele katika njia ya
sala
ya juu kabisa, hata akaweza kuielekeza kwa kufafanua hatua zake.
Mwaka
1591
aliondolewa ma
jukumu
yote na kupangiwa aende katika kanda mpya ya
Meksiko
barani
Amerika
. Akiwa anajiandaa kwa
safari
hiyo ndefu pamoja na wenzake 10, tarehe
28 Septemba
1591
akiwa
mgonjwa
alisafiri kwenda kujifungia katika konventi ya
Ubeda
(karibu na
Jaen
), alipozidi kuugua kwa mateso makali na
uvumilivu
mkubwa hadi alipofariki usiku kati ya tarehe
13
na
14 Desemba
1591
.
Wakati wenzake walipokuwa wanaimba
Kipindi cha Masomo
, aliaga, “
Leo
naenda kuimba
Masifu
mbinguni
”.
Masalia
yake yalihamishiwa Segovia.
Roho yangu ni kavu ndani mwangu
kwa sababu imesahau kujilisha wewe.
Pamoja na kuwa
mshairi
, Yohane alikuwa hasa
mwanateolojia
, aliyetunga vitabu mbalimbali kuhusu
maisha ya Kiroho
, yaani
sala
na safari ya kumuelekea
Mungu
kwa njia ya mkato (kupitia
hatua ya utakaso
,
hatua ya mwanga
na
hatua ya muungano
).
Kufuatana na
mapokeo
ya
Ukristo
, alifundisha namna ya kubandukana na wote na vyote ili kuungana na Mungu tu aliye kwa pamoja ≪mwanga wenye giza na giza angavu≫, kwa kuwa mwanga wake ni mkali mno kwa macho yetu mabovu.
Mojawapo ya semi zake ilikuwa kwamba: ≪Mungu anamnyenyekesha sana mtu ili kumuinua sana≫.
Maandishi na sifa yake baada ya kifo
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Maandishi yake ni kama ifuatavyo:
- Wimbo wa Kiroho
- Usiku wenye giza wa roho
- Kupanda mlima Karmeli
- Mwali hai wa upendo
- Mawazo juu ya upendo na amani
- Barua
Katika “Wimbo wa Kiroho”, Yohane anaeleza maendeleo ya
utakaso
wa
roho
kama njia ya kuzidi kumpata Mungu kwa
furaha
, hadi mtu anapotambua kwamba anampenda kwa
upendo
uleule ambao anapendwa naye.
“Mwali Hai wa Upendo” kinaendeleza
mada
hiyo kwa kufafanua zaidi hali ya
muungano na Mungu
unaomgeuza mtu ndani yake. Mfano unaotumika tena na tena ni ule wa
moto
: kama vile huo unavyozidi kuwaka kwa
nguvu
na kushika
ukuni
hata kuugeuza
mwali
,
Roho Mtakatifu
naye, kisha kutakasa roho katika usiku wenye
giza
, anaiangaza na kuiwasha kama mwali wa moto. Maisha ya roho ni
adhimisho
la mfululizo la Roho Mtakatifu ambalo mtu anaanza kuonja utukufu wa kuungana na Mungu
milele
.
“Kupanda Mlima Karmeli” kinaelekeza roho katika utakaso wake wa hatua kwa hatua, unaohitajika ili kupanda hadi vilele vya
ukamilifu
wa Kikristo, unaomaanishwa na
mlima
huo. Utakaso huo unapendekezwa kama safari ambapo mtu anashirikiana na Mungu ili kubandukana na lolote lililo kinyume na matakwa yake matakatifu. Utakaso huo, unaotakiwa kuwa kamili uweze kufikia muungano wa upendo na Mungu, unaanza na
hisi
, halafu unaendelea na
maadili ya Kimungu
(
imani
,
tumaini
na upendo) ili kutakasa pia
akili
,
kumbukumbu
na
utashi
.
“Usiku Wenye Giza wa Roho” kinafafanua
kazi
ya Mungu mwenyewe katika kuitakasa kikamilifu roho ya mtu na kuiandaa iweze kuungana naye kwa upendo. Hiyo inahitajika kwa sababu
juhudi
za
binadamu
haziwezi kutosha kufikia mizizi mirefu ya maelekeo na mazoea mabaya aliyonayo. Mtu anaweza kuyadhibiti, lakini si kuyang’oa kabisa. Hiyo ni kazi ya Mungu tu: mtu anapaswa kukubali afanyiwe, lakini ni Roho Mtakatifu ambaye kama mwali wa moto anateketeza
uchafu
wowote. Katika hali hiyo mtu anajaribiwa kwa kila namna, kama kwamba angejikuta katika usiku wenye giza nene.
Mihtasari hiyo ya vitabu muhimu zaidi vya Yohane wa Msalaba inatusaidia kutambua mafundisho yake makuu kuhusu
maisha ya Kiroho
, yaliyoelekeza kwa hakika njia ya
utakatifu
ambao Mungu anawaitia wote,
Kwake viumbe vyote ni vyema, na kwa kuvipitia tunaweza kumfahamu
Muumba
aliyeacha
athari
yake ndani ya hivyo vyote. Lakini ni imani tu inayotuwezesha kumjua Mungu jinsi alivyo kwa ndani, yaani katika
umoja
wa Nafsi tatu. Yale yote aliyotaka kuwashirikisha binadamu aliyatoa katika
Yesu Kristo
, Neno wake aliyefanyika mwili: ndiye njia pekee ya kumfikia
Baba
.
Viumbe vyote si kitu kabisa vikifananishwa na Mungu, kwa hiyo ili tufikie
upendo kamili
wa Mungu, ni lazima ma
pendo
mengine yote yalinganishwe nao ndani ya
Kristo
. Ndiyo sababu Yohane anasisitiza haja ya utakaso na
uvuaji
kamili ili kugeuzwa ndani ya Mungu, lengo la ukamilifu.
Safari ndefu na ngumu ya utakaso inadai juhudi za mtu, lakini mtendaji mkuu ni Mungu: mtu anapaswa hasa kujiandaa afanyiwe kazi bila kuizuia. Hasa atekeleze maadili ya Kimungu ambayo yanakua pamoja na maendeleo ya utakaso na muungano na Mungu, hadi mtu ageuzwe ndani ya Mungu.
Akifikia lengo hilo, mtu anazama ndani ya
Utatu Mtakatifu
na kumpenda Mungu kwa upendo uleule anaopendwa naye, yaani anampenda kwa Roho Mtakatifu. Anajisikia amezama katika upendo wa Mungu na kuufurahia bila
kipimo
. Anafahamu yote kumpitia Mungu, asihitaji tena kuvipitia viumbe ili kumfikia.
Maandishi yake yalitolewa kwa mara ya kwanza mwaka
1618
, akatangazwa na
Papa Klementi X
kuwa
mwenye heri
tarehe
25 Januari
1675
, halafu
mtakatifu
na
papa Benedikto XIII
tarehe
27 Desemba
1726
na hatimaye
mwalimu wa Kanisa
na
Papa Pius XI
tarehe
24 Agosti
1926
.
Kulinganisha maandishi yake na yale ya Teresa wa Yesu
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Tangu tusome mara ya kwanza maandishi ya Teresa wa Yesu na Yohane wa Msalaba, ni rahisi tutambue tofauti ambazo zimesisitizwa mara nyingi. Zinatokana na tofauti za mitazamo yao.
Teresa alitegemea mang’amuzi yake binafsi, akidokeza
neema
za pekee alizojaliwa (
njozi
n.k.) asiwe makini kuzitofautisha na mambo yaliyo ya lazima katika “makao saba” ya jumba la Kiroho. Hivyo alitia maanani kuliko wengine matukio ya kihisi, ya nje na ya ziada yanayoweza yakaendana na
sala ya kumiminiwa
; vilevile alisisitiza kuzingatia
ubinadamu
wa
Yesu
.
Yohane pia alisema kwa mang’amuzi yake binafsi na ya watu aliowaongoza, lakini hakuyataja, akijitahidi kuyachimba kiteolojia, jambo ambalo ni muhimu ili kutofautisha yaliyo ya kawaida na yaliyo ya ziada. Alieleza sababu za hali mbalimbali za sala kwa mafundisho juu ya
maadili ya Kimungu
na ya
vipaji vya Roho Mtakatifu
vinavyoendana nayo.
Kwa mtazamo huo alizingatia yaliyo ya lazima katika safari ya kuelekea
utakatifu
, hasa
matakaso ya Kimungu
yanayohitajika kwa
usafi
kamili wa
upendo
. Hivyo hakuelekea kujali neema za pekee zinazoendana pengine na sala ya kumiminiwa, wala hakusisitiza kuzingatia ubinadamu wa Yesu, akilenga moja kwa moja shabaha kuu ya sala, yaani
Mungu
aliyemo mwetu, tunayemfikia katika giza la
imani
kwa njia ya ujuzi ambao anatumiminia na unafanana na mang’amuzi.
Kwa kufanya hivyo amekamilisha maandishi ya Teresa na kutusaidia tuyaelewe.
Hata hivyo, chini ya tofauti hizo kuna msingi mmoja, kwa kuwa Teresa alijua vya kutosha mang’amuzi ya wafuasi wake aweze kuelewa na kueleza nini inatokea kwa kawaida kwa watu wanaopitia hayo makao saba. Tukitumia maelekezo aliyoyatoa huko na huko tunaweza kubainisha zaidi yaliyo ya lazima na yaliyo ya ziada.
Kimsingi watakatifu hao walielewa vilevile sala ya kumiminiwa,
muungano na Mungu
unaotokana nayo, na matakaso ya Kimungu yanayohitajika ili kuufikia ule kamili.
Ikifaa kuonyesha tofauti zao, inafaa zaidi kuonyesha wanavyolingana na kutambua
teolojia
inavyoweza kusaidia katika masuala hayo magumu.
- Dark Night of the Soul: A Masterpiece in the Literature of Mysticism
(Translated and Edited by E. Allison Peers),
Doubleday
, 1959.
ISBN 978-0-385-02930-8
- The Poems of Saint John of the Cross
(English Versions and Introduction by
Willis Barnstone
),
Indiana University Press
, 1968, revised 2nd ed.
New Directions
, 1972.
ISBN 0-8112-0449-9
- Dark Night Of The Soul, Saint John of The Cross
(Translated by Mirabai Starr),
Riverhead Books
, New York, 2002,
ISBN 1-57322-974-1
- Poems of St John of The Cross
(Translated and Introduction by
Kathleen Jones
),
Burns and Oates
, Tunbridge Wells, Kent, UK, 1993,
ISBN 0-86012-210-7
- The Collected Works of St John of the Cross
(Eds. K. Kavanaugh and O. Rodriguez), Washington DC, 1964
- Sr. Pascale-Dominique Nau,
When God Speaks: Lectio Divina in Saint John of the Cross and the Ladder of Monks
(Rome: Lulu.com, 2011)