Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Windows XP
ni toleo la mfumo wa kazi wa
tarakilishi
uliokuwa miongoni mwa
Windows
zenye kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko zile za zamani, kama Windows 95, Windows 98 na Windows Millenium.
- Wepesi wa kuanza na kumaliza kutumia.
- Uwezo wa kutumia
lugha
mbili, kwa mfano
Kiingereza
na
Kiarabu
, pia uwezo wa kubadilisha lugha hizo na kuweka nyengine.
- Kufungua kurasa kwa haraka.
- Uwezo wa kuendesha
programu
zaidi ya moja kwa wakati mmoja.
- Uwezo wa kuhifadhi vitufe (files) vilivyofutwa katika kapu (recycle bin).
- Uwezo wa kufanya kazi katika
mdahalishi
(network) kwa haraka.
- Uwezo wa kubadilishana vitu (data) kati ya programu tofauti.
- Kutumia majina marefu (zaidi ya
herufi
255 katika jina la faili moja).
- Haraka na wepesi katika utekelezaji.
- Vifaa vya kisasa vinavyowezesha kufanya kazi katika net.
- Uwezo wa kutambua
idadi
nyingi za vyombo vilivyounganishwa ndani ya kumpyuta.
- Uwepo wa
picha
nyingi zenye kuvutia kwa ajili ya kupamba skirini (Backgrounds).
Kabla hujaanza kutumia Windows unatakiwa kufanya mambo yafuatayo:
- 1. Kuhakikisha waya wa umeme umeshaunganishwa kwenye kompyuta yako.
- 2. Kufungua kompyuta kwa kutumia sehemu inayoitwa power.
- 3. Kusubiri mpaka idhihiri sehemu inayoitwa desktop.