Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pande mbili za
Papyrus Bodmer VIII
, nakala ya zamani zaidi ya 2Pet tuliyonayo.
Waraka wa pili wa Petro
ni kimojawapo kati ya
vitabu
27 vya
Agano Jipya
katika
Biblia ya Kikristo
.
Kama vitabu vingine vyote vya
Biblia
, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa
historia ya wokovu
ili kukielewa kadiri ya
maendeleo
ya
ufunuo
wa
Mungu
kwa
binadamu
.
Siku hizi
wataalamu
wanakubaliana kukanusha
barua
hiyo kuwa imeandikwa kweli na
Mtume Petro
, wakisema ni kitabu cha mwisho kuandikwa katika
Agano Jipya
(labda huko
Roma
mwaka
100
hivi
B.K.
).
Kwa hakika iliandikwa baada ya
waraka wa Yuda
, kwa sababu inatumia
maneno
yake mengi.
Inawezekana
mwandishi
alitumia vilevile maneno ya Petro ambayo sasa yamepotea; kwa vyovyote aliandika kwa
mamlaka
yake kwa
makanisa
yote ili kuthibitisha
mapokeo
.
Pamoja na kupinga
uzushi
, lengo la barua ni kueleza sababu gani
Bwana
anachelewa kurudi
.
Mafundisho mengine muhimu yaliyomo yanahusu
uvuvio
wa
Roho Mtakatifu
juu ya
waandishi
wa
Biblia
(
Paulo
mmojawao),
wito
wetu wa kushiriki
umungu
, uwepo wa
ulimwengu mpya
baada ya huu wa sasa kuangamizwa (2Pet 1:3-11,19 21; 3:8-18).
- Adams, Thomas B. "A Commentary on the Second Epistle General of Second Peter" Soli Deo Gloria Ministries, 1990.
ISBN 978-1-877611-24-7
- Green, Michael. "The Second Epistle of Peter and The Epistle of Jude: An Introduction and Commentary"
Wm. B. Eerdmans Publishing Company
, 2007.
ISBN 978-0-8308-2997-2
- Leithart, Peter J. "The Promise Of His Appearing: An Exposition Of Second Peter"
Canon Press
, 2004.
ISBN 978-1-59128-026-2
- Lillie, John. "Lectures on the First and Second Epistles of Peter" Klock & Klock Christian Pub, 1978.
ISBN 978-0-86524-116-9
- Seton, Bernard E. "Meet Pastor Peter: Studies in Peter's second epistle" Review and Herald Pub. Association, 1985.
ISBN 978-0-8280-0290-5
|
Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Waraka wa pili wa Petro
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|