Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wandali
ni
kabila
linalopatikana hasa
kusini
magharibi
mwa nchi ya
Tanzania
, katika
Wilaya ya Ileje
,
Mkoa wa Songwe
. Kabla
mkoa
huo haujaanzishwa ilikuwa
wilaya
ya
mkoa
wa
Mbeya
. Pia wako nchini
Malawi
.
Ni kabila la watu wapole na wakarimu sana kwa wageni, pia lenye
juhudi
sana kwa
kazi za mikono
, mathalani, kulima kwa
jembe
la mikono na kupasua
mbao
kwa
msumeno
wa mikono.
Hii pia inachangiwa kwa kiasi kikubwa na
jiografia
ya
wilaya
hiyo kuwa na miinuko mingi kwa sehemu kubwa, hasa kwa ukanda wa Undali yaani ukanda ambao wilaya ya Ileje inapakana na
wilaya ya Rungwe
na
wilaya ya Kyela
.
Wanadumisha sana
lugha
yao, ambayo inaitwa
Kindali
na inafanana na
Kinyakyusa
. Hii ni kwa sababu kabila la Wandali kwa
asili
,
historia
ya masimulizi ya watu wa zamani inaonyesha kuwa na
chimbuko
moja na kabila la
Wanyakyusa
. Tofauti kati ya makabila hayo mawili hutokana na utengano wa watu wa zamani kijiografia tu.
Wanawake wa Kindali ni watu wastaarabu sana, wachapakazi na wenye mapenzi ya kweli na dhati: pesa kwao ni hitaji la mwisho kabisa baada ya namba moja ambayo ni mapendo.
Upande wa
dini
wengi wao ni
Wakristo
, hasa wa
madhehebu
ya
Wamoravian
.
Chakula
chao kikuu ni
ugali
wa
mahindi
, pamoja na
ndizi
, ma
parachichi
na
magimbi
bila kusahau
viazi vitamu
na
mihogo
. Pia hujishughulisha na
ufugaji
wa
ng'ombe
,
mbuzi
,
kondoo
na
kuku
, na
ususi
wa
nyungo
ambao umekuwa sehemu muhimu ya
biashara
ndani na nje ya mkoa.
|
Makala hii kuhusu utamaduni wa
Tanzania
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Wandali
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|