Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wameru
wa
Tanzania
(au "Warwa") ni
kabila
la
watu
wa
Kibantu
wa
jamii
ya
Wachaga
wanaoishi hasa kwenye
Mlima Meru
katika
Mkoa wa Arusha
,
kaskazini
mwa nchi ya
Tanzania
.
Lugha
yao ni
Kirwa
[1]
.
Wanakadiriwa kuwa
milioni
2, wengi wao wakifuata
dini
ya
Ukristo
.
Mbali na
jina
, Wameru hao ni tofauti kabisa na
Wameru wa Kenya
kwa
historia
na
utambulisho
. Sanasana ni kwamba pande zote mbili ni
wakulima
wenye bidii kubwa
[2]
.
Inasemekana Wameru walifikia mlima huo miaka 800 hivi iliyopita wakitokea
milima
ya
Usambara
,
Mkoa wa Tanga
. Walikuta huko
wawindaji
walioitwa
Wakoningo
ambao walikuja kumezwa na jamii ya Wameru.
[3]
Taarifa nyingi kuwahusu Warwa (Wameru) zinapatikana katika
kitabu
kiitwacho "Mountain Farmers-Moral Economies of Land & Agricultural Development in Arusha & Meru" kilichoandikwa na Prof. Thomas T. Spear.
|
Makala hii kuhusu utamaduni wa
Tanzania
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Wameru (Tanzania)
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|