Lebo
ya Umasoni inahusiana na asili ya chama kati ya wajenzi.
Kuingizwa
katika chama cha Wamasoni
karne XVIII
. Lengo la
ibada
hiyo ni kuachana na maisha ya awali kwa kuigiza
kifo
na
kuzaliwa upya
katika maisha ya wanachama.
Jengo la Palazzo Roffia,
Florence
lililotengenezwa kwa ajili ya kufuata taratibu za Kifaransa za kisasa.
Wamasoni
(vilevile
Masunia
; kwa
Kiingereza
Freemasons
yaani
Waashi huru
) ni
chama
cha
siri
kinachodai kufuata
maadili
na kustawisha
udugu
kati ya watu huru.
Msingi wake ni
agano
kati ya wanachama kwa ajili ya kushirikiana ili kufikia malengo ya pamoja.
Wamasoni wanatamka rasmi kutokuwa na
ubaguzi
wowote kati yao na kwa wanaotaka kujiunga nao, kufuatana na taratibu zilizopangwa katika
Katiba ya waashi huru
ambayo iliandikwa na
James Anderson
mwaka
1723
na inakubaliwa na miundo yote ya Kimasoni
duniani
ingawa kati yake kuna tofauti kadhaa kadiri ya mazingira.
Asili ya chama hicho haijulikani kwa hakika, hasa kabla ya mwaka
1650
. Vilevile siri inayotawala maisha ya chama, hata kati ya ngazi mbalimbali za waliojiunga, inafanya iwe vigumu kuelewa malengo halisi na
mbinu
zinazotumika kuyafikia duniani kote.
Chama kinafanana na
dini
yenye
madhehebu
na
ibada
, hata kumbi zake zinaitwa ma
hekalu
.
Mungu
anaitwa kwa kawaida
Msanii majengo mkuu
wa
ulimwengu
.
Wakatoliki
(na baadhi ya
Wakristo
wengine) hawaruhusiwi kujiunga na chama hicho.
Asili ya Wamasoni
Asili ya Wamasoni ilikuwa katika
jumuiya
ya
waashi
yaani ma
fundi
waliojenga makanisa makubwa ya
Ulaya
wakati wa
zama za kati
. Wakati ule mafundi wa
fani
mbalimbali walipaswa kuwa wanachama wa jumuiya ya
ufundi
wao. Jumuiya hizo zilitunza
elimu
yao kama siri na wanachama walipaswa kuahidi kutunza siri za ufundi wao pamoja na siri za jumuiya. Wote walitakiwa kusaidiana.
Mkutano wa Wamasoni, Paris, 1745.
Wakati wa kupokelewa, mwanachama mpya alitoa
kiapo
kilichofuatwa na viapo vingine baada ya kupanda ngazi katika ufundi wake.
Jumuiya hizo mara nyingi zilikuwa na
salamu
na maneno ya siri zilizosaidia kujtambulisha kama ndugu wa jumuiya wakati wa kufika katika
mji
mwingine.
Katika jamii ya Ulaya ya zama za kati jumuiya zote za mafundi zilikuwa pia na tabia ya kidini; kila mwanachama alipaswa kuwa Mkristo
[1]
; kwa kawaida kila jumuiya ilijiweka chini ya ulinzi wa
mtakatifu
fulani na kuanza mikutano yao kwa sala na ibada. Mfumo huu wa ufundi ulikwisha polepole.
Katika
Uingereza
jumuiya za waashi ziliendelea hata wakati ujenzi wa makanisa makubwa ulikuwa umepungua na elimu ya ufundi ilisambazwa zaidi tangu kuwepo wa
uchapaji
vitabu. Waashi walianza kupokea wanachama wasiokuwa wajenzi lakini waliendelea kujiita "Waashi huru".
Uhusiano kati ya jumuiya za waashi na Ukristo ulibadilika kutokana na
matengenezo ya Kiprotestanti
kwa sababu viongozi wa Kiprotestanti walijaribu kupiga
marufuku
jumuiya za mafundi zilizoendelea na ibada zenye tabia nyingi za Ukatoliki kati yao. Hata hivyo jumuiya za waashi ziliweza kuendelea kutokana na umuhimu wa ufundi wao.
Maandamano
kwenye siku za watakatifu yalizuiliwa.
Wakati wa
zama za mwangaza
fikra za
falsafa
mpya zilienea na jumuiya za waashi ziliwapa wanachama wao nafasi ya kujadili fikra hizo kwa
uhuru
zaidi kuliko
jamii
kwa jumla kwa sababu ya tabia ya kisiri ya mikutano yao. Hapo mawazo ya "dini ya kimantiki" yalitokea na kwa jumla waashi huru kati yao waliunda ibada zilizokazia maadili mema bila kutaja tena mafundisho ya Kikristo hasa. Wanachama walipaswa kukiri
imani
katika "roho mkuu" bila kutumia tena
lugha
ya kikristo au kukubali mafundisho ya Kanisa. Walilenga kuunganisha Wakristo wa madhehebu mbalimbali pamoja na Wayahudi na watu waliokataa imani ya dini yoyote.
Kutoka Uingereza Wamasoni walienea hadi
Ulaya bara
na pia
Marekani
, baadaye pia katika ma
koloni
mbalimbali.
Wanaendelea kutumia vyeo vya kale kwa wanachama. Mgeni anapokewa kama
mwanagenzi
(apprentice)
, anaendelea kuwa fundi
(fellow)
na
mwenyekiti
au
msimamzi
wa jumuiya ya kieneo huitwa
gunge
(master)
. Jumuiya zao za kimahali zinaitwa
nyumba
(lodge)
.
Tanbihi
- ↑
Hii ilikuwa sababu muhimu ya kwamba
Wayahudi
wa Ulaya walizuiliwa kutekeleza kazi nyingi za kifundi maana hawakupokelewa katika jumuiya za mafundi
|
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|