Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uzi wa kioo
(kwa
Kiingereza
: glass fiber, optical fiber)
ni
uzi
mwembamba wa
kioo
au
plastiki
ambao unaweza kupitisha
nuru
kutoka upande mmoja hadi mwingine.
Nyuzi za kioo hutumiwa hasa katika
mawasiliano ya simu
, lakini hutumiwa pia kwa kuangaza
majengo
,
vifaa
vya
upimaji
, na
kamera
maalumu za kuangalilia ndani ya nafasi ndogo. Katika
tiba
huhitajika kuangalia hali ya ndani ya
mwili
bila
upasuaji
, kama vile ndani ya
mishipa ya damu
au ndani ya
utumbo
.
Uzi wa kioo ni
ugwe
mwembamba na mrefu wa kioo kitupu (SiO
2
) ambacho ni kiini. Unafungwa katika
koti
la
mata
tofauti inayosababisha
akisisho
kamili la ndani. Hivyo nuru inabaki ndani ya kiini hadi mwisho wa uzi.
Ikiwa koti la ndani linakwaruzwa, linaweza kuvunjika. Hivyo kuna
matabaka
ya hifadhi nje ya koti hilo yanayolilinda. Yote yanafungwa tena katika koti la nje linalofanya
kebo
yote imara.
Matumizi makuu ya nyuzi za kioo ni katika
mawasiliano ya simu
(telecommunication).
Ishara
za
habari
zinapitishwa ndani ya nyuzi hizo, kimsingi sawa na ishara za
umeme
katika nyaya za
shaba
. Lakini nyuzi za kioo zinaruhusu kiasi kikubwa zaidi cha ishara kupitishwa (
gigabaiti
hadi
terabaiti
kwa
sekunde
), tena kwa
umbali
mkubwa zaidi bila
amplifaya
. Tangu kuanzishwa katika
miaka ya 1970
,
teknolojia
ya nyuzi za kioo imeleta
mapinduzi
katika
mawasiliano
.