Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Utashi
(kwa
Kiingereza
:
will
) ni
kipawa
cha
binadamu
kinachomfanya aweze kutaka mwenyewe chochote.
Kitu hicho kinaweza kuwa chema na hata kibaya, ingawa
akili
yake mwenyewe inaona zaidi wema fulani uliomo na ambao unamvuta.
Katika
dunia
hii binadamu ndiye kiumbe pekee mwenye utashi, nao huongeza sifa ya utambuzi wa mvuto wa kilicho chema katika ubaya au kilicho kibaya katika wema, kuchagua na kupanga kwa kuzingatia yaliyopita na matamanio katika wakati ujao, kuunda mambo mapya, na kutamani kurekebisha mambo kwenda katika hali bora zaidi.