Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uranusi
|
---|
Picha yenye rangi halisi ya Uranusi kama ilivyoonwa na
Voyager 2
mnamo 22 Januari 1986.
|
Ugunduzi
|
---|
Mgunduzi
| William Herschel
|
---|
Tarehe
| 13 Machi 1781
|
---|
Jina
|
---|
Asili ya jina
| Kla.
?ranus
, kutokana na
Kgk.
Ο?ρ?ν?? (
Ouranos
)
|
---|
Alama
| |
---|
Tabia za njiamzingo
|
---|
Umbali mfupi
| km
2,735,560,000
au
18.2861
|
---|
Umbali mrefu
| km 3,006,390,000
au 20.0965
|
---|
| km 2,870,972,000
au 19.19126
|
---|
Uduaradufu
| 0.04717
|
---|
| siku
30,688.5
miaka
84.0205
|
---|
Mwinamo
| 0.773
°
toka
njia ya Jua
|
---|
Miezi
| 27
|
---|
Tabia za kimaumbile
|
---|
| km 25,362±7
mara 3.976 ya Dunia
|
---|
Tungamo
| kg 8.6810×10
25
mara 14.536 ya Dunia
|
---|
| g/cm
3
1.27
|
---|
Uvutano wa usoni
| m/s
2
8.69
|
---|
| km/s 21.3
|
---|
| siku ?0.71832
|
---|
| siku ?0.71833
|
---|
Weupe
| 0.300 (
Bond
)
0.488 (
jiometri
)
|
---|
Halijoto
| K
76 (?197.2
°C
)
|
---|
Kuhusu matumizi ya jina
Zohali
kwa sayari hii tazama kipengele cha "Asili ya jina"
Uranusi
ni
sayari
ya saba kutoka
Jua
.
Asili ya jina
Waswahili wa kale hawakujua sayari hii. Uranusi ni jina la kimataifa lililoteuliwa katika karne ya 19 baada ya majadiliano marefu kati ya wanaastronomia wa Ulaya. Ni jina la mungu wa
Ugiriki ya Kale
Urano
(
Kgi.
Ο?ραν??) aliyeaminiwa kuwa mungu wa anga. Lugha nyingi duniani zimepokea jina hili kwa sababu astronomia ya zamani haikujua sayari hii.
Vitabu kadhaa vinatumia jina la
Kiswahili
Zohali
[1]
[2]
[3]
kwa kufuata kamusi ya
KAST
; lakini hili ni jina la Kiswahili kwa
sayari ya sita
(
Kng.
Saturn
).
[4]
Tabia
Ni sayari kubwa ya tatu ya
Mfumo wa Jua
hata kama mada yake ni hasa gesi iliyoganda. Jumla ya masi yake ni mara 14 ya dunia hivyo ni sayari nyepesi kulingana na ukubwa wake. Kipenyo chake ni takriban kilomita 50,000
[5]
.
Inazunguka Jua kwenye obiti inayochukua miaka 84. Umbali wake na Jua ni takriban mara 19 umbali wa Jua na Dunia au
kilomita
bilioni 2.9;
afeli
yake ni
vizio astronomia
20.11 na
periheli
yake ni vizio astronomia 18.33.
Hadi mwaka 2023 miezi 27 iligunduliwa. Miezi mikubwa huitwa
Miranda
,
Arieli
,
Umbrieli
,
Titania
na
Oberoni
. Ina pia pete kadhaa yaani mawingu ya vumbi, barafu na mawe madogo ambayo ni nyembamba na kuzunguka sayari kwa umbo la pete. Pete za Uranusi ni hafifu kuliko zile za
Zohali
.
Uranusi inaonekana kama nyota hafifu sana yenye
mwangaza
wa 5.6 - 6. Kutokana na kuwa hafifu vile na mwendo wake wa pole hakuna utamaduni wowote wa kale ulioitambua kuwa sayari. Ilitambuliwa mara ya kwanza kuwa sayari na tarehe
13 Machi
1781
na
William Herschel
.
Tazama pia
Marejeo
- ↑
Wallah, W.B. & Mwamburi, J. Kiswahili mufti darasa la 8: Mwongozo wa mwalimu. Longhorn, 2009. ISBN 99966491066
- ↑
TESSA - Teacher Education in Sub Saharan Africa.
Nishati na Mwendo: Kutoka Ardhini kenda kwenye nyota ? kutumia Zana Kifani
Archived
9 Aprili 2016 at the
Wayback Machine
.. Available at: www.tessafrica.net
- ↑
Waweru, M.; Makombo, H; Vonuoli, A.; Kashihiri, C.; Mwayani, J.
Hutua za Kiswahili: Masomo ya Msingi 8
. East African Educational Publishers ltd., 1ed, 290p., 2005.
ISBN 9966-25-403-X
- ↑
KAST ni kamusi ya pekee inayotumia "Zohali" kwa sayari hii. Kamusi za
KKK/ESD
ya
TUKI
na
M-J SES
zinaonyesha "Zohali" kwa sayari ya sita na "Uranus" kwa sayari hii. Linganisha ukurasa wa
Majadiliano:Sayari
- ↑
Uranus - by the numbers
, tovuti ya NASA, iliangaliwa Januari 2021
|
Makala hii kuhusu mambo ya
sayansi
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Uranusi
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|