Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
|
|
|
|
Umwilisho
(kwa
Kiingereza
"incarnation" kutoka
Kilatini
"incarnatio") ni
neno
la
teolojia
linalotumika kulitaja
fumbo
la
imani
ya
Ukristo
la kwamba
Mwana wa Mungu
alijifanya
binadamu
kweli kwa kutwaa
roho
na hata
mwili
kama vile vya mtu yeyote.
Mkazo juu ya mwili unatokana na
dibaji
ya
Injili ya Yohane
inayosisitiza ajabu la tukio hilo ikisema:
"Neno akawa mwili akakaa kwetu"
(1:14).
Kwa
msingi
huo
Kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli
inafundisha kukiri:
Alishuka toka
mbinguni
kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya
wokovu
wetu, akapata mwili kwa uwezo wa
Roho Mtakatifu
kwake yeye
Bikira Maria
akawa mwanadamu
.
Umwilisho ulifanyika pale ambapo Maria alikubali
wito
wa
Mungu
kwake alivyoletewa na
Malaika Gabrieli
katika
kijiji
chake,
Nazareti
. Habari inasimuliwa hivi (
Lk
1:26-38):
26 Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, 27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. 28 Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. 29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? 30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. 31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. 32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. 33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. 34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? 35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. 36 Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; 37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. 38 Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.
Dini
nyingine ziliwahi kusimulia juu ya
mungu
fulani kuja
duniani
akionekana kama mtu (kwa mfano
Avatar
katika
Uhindu
), lakini umwilisho ni wa pekee kwa kuwa unatokana na imani ya kuwa
Yesu
tangu alipotungwa
tumboni
mwa
mama
yake ni binadamu halisi kama mwingine yeyote, ingawa
nafsi
yake ni ya
milele
kama ile ya
Mungu Baba
na ya Roho Mtakatifu.
Imani hiyo inaongoza kumkiri Yesu kuwa Mungu kweli milele yote na mtu kweli tangu alipotwaa mwili. Kwa sababu hiyo, Wakristo wengi (Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na baadhi ya Waprotestanti) wanamuita Maria "
Theotokos
" (yaani "Mzazi wa Mungu" au "
Mama wa Mungu
", kwa maana ni mama aliyemzaa mtu ambaye tangu milele ni Mungu, si kwamba aliweza kumzaa Mungu kama Mungu).
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Umwilisho
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|