Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la Umedi katika Uajemi ya magharibi
Milki ya kimedi mnamo mwaka 600 KK
Askari ya Kimedi (kushoto) na Mwajemi (kulia); kutoka jumba la kifalme cha Apadana
Umedi
ilikuwa nchi na milki ya kihistoria na sehemu kubwa ya eneo lake lilikuwa ndani ya
Uajemi
ya magharibi ya leo.
Kiasili ni jina linalojumlisha makabila mbalimbali yaliyofika katika Iran ya leo mnamo mwaka
2500 KK
. Mnamo mwaka
600 KK
Wafalme wa Umedi waliweza kupanua milki yao na kutawala sehemu kubwa za
Mashariki ya Kati
. Mwaka
539 KK
milki yao ilitwaliwa na
Koreshi Mkuu
na kuendelea kama sehemu ya milki ya Uajemi.
Wafalme wakuu wa Uajemi waliendelea kama "wafalme wa Waajemi na Wamedi" na hivyo jina la Umedi na Wamedi linapatikana mara kadkhaa katika maandiko ya
Biblia ya Kiebrania
.
Mwanahistoria
Strabo
wa
Ugiriki ya Kale
alisema ya kwamba Kimedi na lugha nyingine za Kiajemi zinafanana.
"Jina la
Ariana
linataja maeneo zaidi kuliko
Uajemi
na Umedi, lakini pia
Baktria
na Sogdia upande wa kaskazini; maana hao wote huzungumza takriban lugha moja ingawa kuna tofauti ndogo za kieneo."
[1]
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Umedi
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|