Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ukanda wa Kuiper
(kwa
Kiingereza
Kuiper belt
) ni eneo la
mfumo wa jua letu
nje ya
obiti
ya
sayari
Neptuni
lililopo kwenye
umbali
wa
vizio astronomia
) kati ya 30 - 50 kutoka
jua
.
Ukanda huu una
umbo
la
wingu
wa
mviringo
wa
magimba ya angani
; mengi yao ni madogo, machache makubwa kwa hiyo ukubwa kati ya
vumbi
na
mawe
hadi
asteroidi
na pia
sayari kibete
,
Ukanda wa Kuiper hufanana na
ukanda wa asteroidi
ulipo kati ya obiti za
Mirihi
(Mars)
na
Mshtarii
(Jupiter)
lakini ni kubwa zaidi.
Upana
wake ni mara 20 na
unene
wake mara 20-200.
Magimba ndani yake ni hasa aina mbalimbali za
barafu
kutokana na
elementi
zilizoonekana kama
gesi
katika
mazingira
ya dunia kama vile
methani
,
amoni
au
maji
.
Wataalamu
wanaamini leo ya kwamba chanzo hasa cha magimba ni mchakato wa kutokea kwa mfumo wa jua letu na kuzaliwa kwa sayari. Katika maeneo ya ndani ya mfumo wa jua
mata
ilijikusanya kutokana na
graviti
kuwa ama jua lenyewe au sayari. Hapa nje masi za magimba hazikutosha kuyavuta magimba mengine ili sayari kubwa itokee.
Hata hivyo kuna sayari kibete
tatu
zilizogunduliwa hadi sasa katika ukanda wa Kuiper ambazo ni
Pluto
,
Haumea
na
Makemake
.
Kuna pia
nadharia
ya kwamba
miezi
kadhaa katika mfumo wa jua letu ina
asili
yake katika ukanda wa Kuiper. Mifano ni
Triton
ya
Neptuni
na
Phoebe
ya
Zohali
. Miezi hii inaaminiwa ilijijenga katika ukanda wa Kuiper lakini ilivutwa ndani ya mfumo wa jua na kukamtwa na
graviti
ya sayari hizo.
Ukanda wa Kuiper uligunduliwa
mwaka
1992
lakini iliwahi kutabiriwa na wataalamu mbalimbali pamoja na
Gerard Kuiper
.
Hadi sasa kuna takribani magimba 1,000 yaliyogunduliwa kwa uhakika lakini inaaminiwa ya kwamba jumla ya magimba unaweza kufikia
idadi
ya
malakhi
au
mamilioni
.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
sayansi
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Ukanda wa Kuiper
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|