Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
|
|
|
|
Ujio wa pili
ni
imani
ya kwamba
Yesu
, aliyekuja mara ya kwanza kwa
unyenyekevu
alipozaliwa na
Bikira Maria
, atashuka tena toka
mbinguni
kwa
utukufu
siku ya
kiyama
.
Msingi
wa
tumaini
hilo katika
Ukristo
ni
ahadi
alizotoa mwenyewe na ambazo zinasomwa katika
Injili
(
Math
24:27; 25:31;
Lk
17:30;
Yoh
6:39-40).
Ufafanuzi
zaidi ulitolewa na
Mtume Paulo
(
Mdo
10:42; 17:31;
Rom
2:5-16;
14:10;
1Kor
4:5; 15:23;
2Kor
5:10;
Fil
1:6;
1Tim
6:14;
2 Tim
4:1,8;
Tito
2:13;
1Thes
5:2;
2Thes
1:5; 2:1-9) na wengineo katika
vitabu
vingine vya
Agano Jipya
(
1Pet
4:13;
Yak
5:7) na baadaye.
Katika
Agano Jipya
neno
?πιφ?νεια,
epiphaneia
,
kutokea
, limetumika mara 5 kuhusiana na kurudi kwa
Kristo
,
[1]
kumbe neno παρουσ?α,
parousia
,
kufika
au
kuwepo
, mara 17.
[2]
[3]
Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli
(
karne ya 4
) ilikiri kwamba "atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho".
Hata hivyo Wakristo wanatofautiana kuhusu jambo hilo kadiri ya
madhehebu
yao, lakini pia kadiri ya
rai
binafsi kuhusu maana halisi ya maneno yake.
Kama Yesu mwenyewe alivyotabiri, jambo hilo litaleta udanganyifu mwingi ambao alitaka wafuasi wake wajihadari usiwapate.
Kweli
karne
hata karne walitokea watu kutabiri
mwaka
au hata
tarehe
ya tukio hilo; tena wengine walisema limeshafanyika, kumbe bado.
Yesu alisema, "Hakuna anayejua siku wala saa". Lakini watu hao walijaribu kutumia
namba
za
Biblia
ili kuhesabu itakuwa lini.
Katika
Islam
, ???? (??s?,
Isa
) anaheshimiwa kama
mtume
na
Masihi
aliyetumwa kwa
Waisraeli
(
ban? isr?'?l
) akiwaletea kitabu kipya,
Injili
.
[4]
Quran
inazungumzia ujio wa pili wa huyo Yesu katika
sura
Az-zukhruf
(43:61) kama
ishara
ya
siku ya hukumu
.
[5]
[6]
Pia kuna
Hadithi za Mtume Muhammad
zinazotabiri wazi ujio wake.
[7]
[8]
- Explanatory text in
The New Jerusalem Bible
(1990). Doubleday.
ISBN 0-385-14264-1
- Max Heindel.
How Shall We Know Christ at His Coming?
, May 1913 (stenographic report of a lecture, Los Angeles),
ISBN 0-911274-64-2
- C. S. Lewis
. (1960).
The World's Last Night and Other Essays
.
Harcourt Brace Jovanovich.
ISBN 0-15-698360-5
- Markus Muhling.
Grundinformation Eschatologie. Systematische Theologie aus der Perspektive der Hoffnung
, Vandenhoeck & Ruprecht, Gottingen 2007,
ISBN 978-3-525-03619-8
, 221?241
- James Stuart Russell
.
The Parousia, A Careful Look at the New Testament Doctrine of the Lord's Second Coming
- Emanuel Swedenborg
.
The Consummation of the Age; the Coming of the Lord; and the New Heaven and New Church
, Chapter 14 in
The True Christian Religion Containing the Universal Theology of The New Church Foretold by the Lord in Daniel 7; 13, 14; and in Revelation 21; 1,2
(Swedenborg Foundation 1952)
- Paramahansa Yogananda.
The Second Coming of Christ: The Resurrection of the Christ Within You.
Self-Realization Fellowship, 2004.
ISBN 978-0876125557
|
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Ujio wa pili
kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|