Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hali ya uhuru wa dini nchi kwa nchi (Pew Research Center study, 2009).
Rangi
ya
njano
hafifu inamaanisha vizuio ni vichache, kumbe
nyekundu
inaonyesha kuna vizuio vingi.
Uhuru wa dini
ni mojawapo kati ya
haki za msingi
za kila
binadamu
kutokana na
hadhi
yake inayomtofautisha na
wanyama
. Yaani
akili
yake inamfanya atafute
ukweli
, jambo linalohitaji kuwa huru kutoka kwa mwingine yeyote.
Uhuru
huo unaendana na
wajibu
na
haki
ya kufuata
dhamiri
hasa katika masuala ya
dini
na
maadili
.
Haki hiyo inatajwa katika
Tamko la kimataifa la haki za binadamu
lililotolewa na
Umoja wa Mataifa
mwaka
1948
, ingawa haitekelezwi vizuri katika nchi nyingi, hasa zile zinazofuata
rasmi dini
fulani au zinapinga dini zote.
Haki hiyo inajumlisha haki ya kuwa au kutokuwa na
imani
fulani, kuibadili, kuitekeleza katika
ibada
za binafsi na za pamoja, kuishuhudia kwa maneno na matendo, kuitangaza, n.k. maadamu mtu hatendi
makosa ya jinai
wala hasababishi vurugu katika
maisha
ya
jamii
.
Suala la kukubali haki hiyo katika
sheria
za nchi lilikabiliwa tangu zamani; maarufu ni hasa
Hati ya Milano
iliyotolewa na
Konstantino Mkuu
mwaka
313
ili kuruhusu
Ukristo
katika
Dola la Roma
baada ya miaka karibu 250 ya
dhuluma
.
|
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Uhuru wa dini
kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|