Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ugiriki ya Kale
ni kipindi cha
historia
ambapo
Ugiriki
ulipanuka katika eneo kubwa la
Mediteraneo
na
Bahari Nyeusi
, na kudumu kwa karibu
milenia
moja
, hadi
Ukristo
ulipoanza. Wakati wa
Yesu
,
kitovu
cha
ustaarabu
huo kilikuwa
mji
wa
Aleksandria
(
Misri
).
Unadhaniwa na
wanahistoria
wengi kuwa ni
utamaduni
anzilishi wa
ustaarabu wa magharibi
lakini iliathiri pia elimu ya
Waislamu
.
Wanafalsafa
na
wataalamu
wake wa
fani
mbalimbali waliweka misingi muhimu ya
maendeleo
ya
sayansi
katika
karne
zilizofuata.
Hata baada ya Ugiriki kuingizwa katika
Dola la Roma
, utamaduni wa Kigiriki ulikuwa na
nguvu
kubwa ya ushawishi.
Maendeleo ya
elimu
katika himaya ya Uislamu yalitegemea kwa kiasi kikubwa kazi ya ufasiri wa
vitabu
vya Wagiriki kwenda
lugha
ya
Kiarabu
.
Ugiriki ya kale umeathiri pia
lugha
,
siasa
, mifumo ya
elimu
,
falsafa
,
sayansi
,
sanaa
,
ufundi
sanifu wa
Dunia
ya kisasa, na kuchochea
Mwamko Mpya
katika
Ulaya Magharibi
; na kuchipuka tena katika vipindi mbalimbali vya
uamsho
wa tamaduni za kisasa za Kigiriki, ndani ya
karne ya 18
na
ya 19
katika
Ulaya
na
Amerika
.
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Ugiriki ya Kale
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|