Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1880
ulikuwa wa 24 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 2 Novemba. Upande wa "
Republican Party
",
James Garfield
(pamoja na kaimu wake
Chester Arthur
) alimshinda mgombea wa "
Democratic Party
"
Winfield Scott Hancock
(pamoja na kaimu wake
William Hayden English
).
Garfield akapata kura 214, na Hancock 155. Ramani yaonyesha kura kwa kila
jimbo
.