Ubatizo
ni
sakramenti
ya kwanza ya
Ukristo
. Unaitwa "mlango wa sakramenti", kwa sababu ni lazima kuupokea kabla ya kupokea nyingine yoyote, hasa
ekaristi
.
Sakramenti ya kwanza daima ni ubatizo, kwa kuwa ndio kupata
uzima mpya
kwa kushiriki
kifo
na
ufufuko wa Yesu
, inavyodokezwa wazi zaidi mtu akizamishwa na kutolewa majini. “Je, hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika
mauti
yake, kusudi kama
Kristo
alivyofufuka katika wafu kwa njia ya
utukufu
wa
Baba
, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa
uzima
. Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kuunganika naye; tukijua nano hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena” (
Rom
6:3-6).
Sakramenti nyingine zote ama zinastawisha ama zinafufua uzima huo wa Kimungu ambao ni sharti la kuingia mbinguni. “Amin, Amin, nakuambia: Mtu asipozaliwa kwa
maji
na kwa Roho, hawezi kuuingia
ufalme wa Mungu
” (
Yoh
3:5).
Kwa hiyo kubatizwa ni kuzika utu wa kale "maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo" (
Gal
3:27).
Ubatizo huonyesha mambo muhimu matatu:
- Kuifia dhambi.
- Kuzaliwa upya katika Kristo.
- Kumpokea Kristo milele.
Ubatizo ni lazima uendane na imani ya kweli. Maana wote wenye imani ya kweli ni watoto wa Mungu: “Kwa maana kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huko ndiko kuushinda ulimwengu, hiyo imani yetu” (
1Yoh
. 5:4).
Jina la
Kiswahili
na la
lugha
nyingine nyingi linatokana na kitenzi cha
Kigiriki
βαπτ?ζω (
baptizo
, maana yake
nazamisha (nazika, nafunika) majini
,
naosha
, lakini pia
nanawa
).
Maana ya kwanza inadokeza lengo la kumzika mtu ili afufuke pamoja na
Yesu Kristo
katika uzima mpya.
Maana ya pili na ya tatu zinadokeza lengo la kumtakasa mtu kutoka
dhambi
zake.
Ibada zinazotumia maji zinapatikana katika
dini
nyingi, kutokana na kitu hicho kumaanisha wazi uzima na
usafi
.
Ubatizo unafanyika kwa maji kwa kuwa ndiyo
ishara
ya usafi na ya uhai unaotupatia kwa uwezo wa
Roho Mtakatifu
. “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na
vinyago
vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi
moyo mpya
, nami nitatia
roho mpya
ndani yenu” (
Ez
36:26-27). “Kisha akanionyesha
mto
wa
maji ya uzima
, wenye kung’aa kama
bilauri
, ukitoka katika
kiti cha enzi
cha
Mungu
, na cha
Mwanakondoo
” (
Ufu
22:1).
Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu mwanzo wa
Kanisa
. Kutokana na umuhimu wa sakramenti hiyo
Yesu
ametuagiza twende kubatiza watu duniani kote. Kitabu cha
Matendo ya Mitume
kinaonyesha waamini walivyotekeleza agizo hilo katika
mazingira
mbalimbali, si tu yalipopatikana maji mengi. Hivyo
Mtume Paulo
alipokuwa ndani ya
nyumba
“akasimama akabatizwa” (
Mdo
9:18). Kumbe
Yohane Mbatizaji
hakusogea mbali na
mto Yordani
, akisubiri watu wamuendee kutoka maeneo yote ya nchi ile kame. “Alikuwa akibatiza huko
Ainoni
, karibu na
Salimu
, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele” (Yoh 3:23).
Yohane Mbatizaji
alipotikisa
Wayahudi
wenzake kwa kuhubiri
toba
kandokando ya mto Yordani aliwadai wapokee "ubatizo wa maji" kama ishara ya kuongoka na ya kuwa tayari kumpokea
Masiya
ajaye, atakayebatiza "kwa
Roho Mtakatifu
na
moto
" (
Math
3:11).
Ubatizo uliotolewa na Yohane Mbatizaji haukuwa sakramenti, kwa sababu yeye alikuwa mtangulizi tu wa Yesu,
mwanzilishi
wa sakramenti zote. “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya
toba
; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa
moto
” (Math 3:11). Paulo aliuliza watu, “‘Mlibatizwa kwa ubatizo gani?’ Wakasema, ‘Kwa ubatizo wa Yohane’. Paulo akasema, ‘Yohane alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu’. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu” (Mdo 19:3-5).
Tofauti kubwa kati ya ubatizo wa Yohane na ule wa Yesu ni kwamba sakramenti inategemea
imani
kwa Kristo na kutushirikisha kifo na ufufuko wake. “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” (
Gal
3:27). Ndivyo inavyoondolea dhambi zote na kuingiza katika uzima wa
Utatu Mtakatifu
. Kwa sababu hiyo Yesu aliagiza tubatize “kwa jina la Baba, na
Mwana
, na Roho Mtakatifu” (Math 28:19). Maneno hayo ndiyo muhimu zaidi katika sakramenti hiyo. Maji peke yake, hasa yakiwa mengi, yanaweza kuosha
mwili
, lakini si
roho
. Kumbe ubatizo unaotuokoa “siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la
dhamiri
safi mbele za Mungu” (
1Pet
3:21).
Yesu
alibatizwa na Yohane akiwa na umri wa miaka 30 hivi akithibitisha ubora wa kazi ya mtangulizi wake na utayari wa kubeba
dhambi
za
ulimwengu
kama
mwanakondoo
wa
sadaka
ya
upatanisho
.
Hapo Roho Mtakatifu alimshukia kwa sura ya
njiwa
na
Mungu Baba
alimshuhudia kuwa ndiye
Mwana
wake mpendwa, aliyempendeza kwa
utiifu
wake (
Mk
1:11).
Injili ya Yohane
inashuhudia kwamba Yesu pia alianza kubatiza, tena watu wengi kuliko Yohane, ingawa kwa njia ya wanafunzi wake (Yoh 3:22; 4:1-2). Ubatizo huo ulifanana kabisa na ule wa Yohane na kulenga Wayahudi.
Kumbe baada ya kufufuka aliwaagiza wanafunzi wake wakabatize mataifa yote akifafanua watumie maneno yapi katika ibada hiyo: "Nimepewa
mamlaka
yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu" (Math 28:19).
Mambo muhimu kabla ya mtu mzima kubatizwa
[
hariri
|
hariri chanzo
]
- Mtu mzima huanza kwa kulisikia
neno la Mungu
; kwa maana "imani huja kwa kusikia" (Rum 10:17).
- Ni lazima kujifunza mambo unayopaswa kuyafanya ili kuikuza imani hiyo. "Enendeni mkayafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza ... na kuwafundisha kuyashika yote niliyoyaamuru mimi" (Math 28:19,20).
- Kisha fanya uamuzi sahihi wa kumfuata Kristo kimaisha.
- Ni lazima kupata toba na msamaha wa dhambi. “Tubuni mkabatizwe kila mtu kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi” (Mdo 2:38).
Kadiri ya
madhehebu
mengi, watoto wachanga wanaweza kubatizwa kwa sababu hawakatai
neema
ya Mungu. Wanafunzi wa Yesu walipotaka kuwazuia wasiletwe kwake “alichukizwa sana, akawaambia, ‘Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa
ufalme wa Mungu
ni wao. Amin, nawaambieni: Yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa” (Mk 10:14-15).
Yeremia
aliambiwa, “Kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa
nabii
wa mataifa” (
Yer
1:5). Yohane Mbatizaji alitabiriwa “atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye” (
Lk
1:15).
Ingawa watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika, Mungu anaweza kuwamiminia rohoni mwanga wa imani. “Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao umeiweka misingi ya nguvu” (
Zab
8:2). “
Elisabeti
aliposikia kule kuamkia kwake
Mariamu
, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake... kwa shangwe” (Lk 1:41,44). “Nakushukuru, Baba, Bwana wa
mbingu
na
nchi
, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye
hekima
na
akili
, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako” (Math 11:25-26).
Hata watu wazima hawawezi kuelewa sakramenti kwa dhati, kwa kuwa zote ni ma
fumbo
yanayotuzidi. Basi, kama
Mtume Petro
alipooshwa miguu, tumuachie
Bwana
atufanyie kazi anavyojua yeye. “Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye” (Yoh 13:7). Kisha kuoshwa tuzidi kuchimba mafumbo hayo kwa mwanga wa
Neno
na wa Roho Mtakatifu. “Je, mmeelewa na hayo niliyowatendea?... Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo” (Yoh 13:12,15).
Kumbe, imani ya watu wazima inaweza kufaidisha watoto kama wengine pia. Walimletea Yesu “mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne... Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, ‘Mwanangu, umesamehewa dhambi zako” (Mk 2:5). Kwa ubatizo watoto wanaunganishwa naye na kuanza kuponywa madonda ya dhambi ya asili. “Tazama, mimi naliumbwa kati hali ya
uovu
, mama yangu alinichukua
mimba
hatiani” (Zab 51:5). “Ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha
haki
, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo” (Rom 5:19).
Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu mwanzo, usipingwe na yeyote kwa miaka elfu na zaidi. Ni kwamba
Wayahudi
walipokea watoto katika dini yao kwa
kuwatahiri
siku ya nane baada ya kuzaliwa. “Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu” (Lk 2:21). Watu wa mataifa walipoongokea dini hiyo, walioshwa na kutahiriwa pamoja na watoto wao.
Mitume
pia walipokea katika Kanisa
familia
nzima, si wazazi tu. Walibatizwa “yeye na nyumba yake”, “yeye na watu wake wote” (Mdo 16:15,33); “watu wa nyumbani mwa
Stefana
” (
1Kor
1:16).
Kadiri ya
Wakatoliki
na
Waorthodoksi
, ubatizo hautoshi, bali unahitaji kukamilishwa na
kipaimara
na
ekaristi
, kama vile baada ya kuzaliwa tunahitaji kukomaa na kudumisha uhai wetu kwa
chakula
. Sakramenti hizo tatu kwa pamoja ni msingi wa maisha ya Wakristo wote, kumbe nyingine zinahitajika tu katika hali na nafasi maalumu. Mitume waliwaendea
Wasamaria
“wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu” (Mdo 8:15-16). “Amin, amin, nawaambieni: Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu” (Yoh 6:53).
- Canadian Council of Churches, Commission on Faith and Witness (1992).
Initiation into Christ: Ecumenical Reflections and Common Teaching on Preparation for Baptism]
(PDF)
. Winfield, B.C.: Wood Lake Books.
ISBN
2-89088-527-5
.
- Chaney, James M.
(2009).
William the Baptist
. Oakland, TN:
Doulos Resources
. uk. 160.
ISBN
978-1-4421-8560-9
.
OCLC
642906193
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo Julai 8, 2009.
{{
cite book
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
)
- Dallmann, Robert (2014).
Baptisms - One? Many? Or Both?
. ChristLife, Inc.
ISBN
978-0991489107
.
- Gerfen, Ernst (1897).
"Baptizein": the Voice of the Scriptures and Church History Concerning Baptism
. Columbus, Ohio: Press of F.J. Heer.
- Guelzo, Allen C (1985).
Who Should Be Baptized?: a Case for the Baptism of Infants
. Reformed Episcopal Pamphlets. Philadelphia, PA: Reformed Episcopal Publication Society.
. 26 pp. N.B.: States the Evangelical Anglican position of the Reformed Episcopal Church.
- Guelzo, Allen C (1985),
What Does Baptism Mean?: a Brief Lesson in the Spiritual Use of Our Baptisms
, Reformed Episcopal Pamphlets, Philadelphia, PA: Reformed Episcopal Publication Society
- Jungkuntz, Richard (1968).
The Gospel of Baptism
. St. Louis: Concordia Publishing House.
OCLC
444126
.
- Kolb, Robert W. (1997).
Make Disciples, baptizing: God's gift of new life and Christian witness
. St. Louis: Concordia Seminary.
ISBN
0-911770-66-6
.
OCLC
41473438
.
- Linderman, Jim (2009).
Take Me to the Water: Immersion Baptism in Vintage Music and Photography 1890?1950
. Atlanta: Dust to Digital.
ISBN
978-0-9817342-1-7
.
- Matzat, Don (Spring 1997).
"In Defense of Infant Baptism"
.
Issues, Etc. Journal
.
2
(3)
. Iliwekwa mnamo
Februari 26,
2009
.
{{
cite journal
}}
: CS1 maint: date auto-translated (
link
)
- Root, Michael; Saarinen, Risto, whr. (1998).
Baptism and the Unity of the Church
. Grand Rapids, MI: W.B. Eerdmans; Geneva: W.C.C. [i.e. World Council of Churches] Publications. Also mentioned on t.p.: "Institute for Ecumenical Research, Strasbourg, France".
ISBN
2-8254-1250-3
.
- Scaer, David P. (1999).
Baptism
. St. Louis: The Luther Academy.
OCLC
41004868
.
- Schlink, Edmund (1972).
The Doctrine of Baptism
. St. Louis, Mo: Concordia Publishing House.
ISBN
0-570-03726-3
.
OCLC
228096375
.
- Slade, Darren M. (Agosti 15, 2014).
"The Early Church's Inconsequential View of the Mode of Baptism"
(PDF)
.
American Theological Inquiry
.
7
(2): 21?34. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo Septemba 3, 2014.
- Stookey, Laurence Hull (1982).
Baptism, Christ's act in the church
. Nashville, TN: Abingdon.
ISBN
0-687-02364-5
.
OCLC
7924841
.
- Torrell, Jean-Pierre (2011).
A Priestly People: Baptismal Priesthood and Priestly Ministry
. New York/ Mahwah, NJ: Paulist Press.
ISBN
978-0-8091-4815-8
.
- Ware, Kallistos
(1993).
The Orthodox Church
. New York: Penguin Books. ku.
277
?278.
ISBN
0-14-014656-3
.
OCLC
263544700
.
- Weigel, George (2016).
"The Most Important Day of Your Life"
.
First Things
.
- Willimon, William H.
(1980).
Remember who you are: baptism, a model for Christian life
. Nashville: Upper Room.
ISBN
0-8358-0399-6
.
OCLC
6485882
.
- World Council of Churches (1982).
Baptism, Eucharist, and ministry
. Geneva:
World Council of Churches
.
ISBN
2-8254-0709-7
.
OCLC
9918640
.
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Ubatizo
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|