Rasi ya Uarabuni
(au:
Bara Arabu
) ni
rasi
kubwa iliyoko
Asia ya Magharibi
kati ya
Bara
la
Afrika
na Bara la
Asia
ambapo sehemu yake kubwa imezungukwa na
bahari
, upande wa
magharibi
Bahari ya Shamu
, upande wa
kusini
na
Bahari ya Hindi
na ule wa
Mashariki
Ghuba ya Uajemi
. Sehemu za
Kaskazini
mwa Bara Arabu zimepakana na nchi za
ufalme
wa
Jordani
na
jamhuri
ya
Iraq
.
Kwa macho ya
gandunia
rasi hii ni karibu sawa na
bamba la Uarabuni
.
Kwa sababu ya
ukame
, hakuna
mito
ya kudumu katika bara hili, ijapokuwa kwenye sehemu mbalimbali kunapatikana
chemchemi
na vijito vya
maji
ambavyo huzidi wakati wa
msimu
wa
mvua
katika
majira ya baridi
. Sehemu kubwa ni
jangwa
tu.
Bara Arabu ina
milima
upande wa Magharibi na Kusini, lakini kila ukiteremkia Mashariki unakutana na
ardhi
tambarare
mpaka kufikia kwenye
Ghuba ya Uajemi
.
Katika
karne ya 20
nchi za Uarabuni zilipata nafasi ya kutajirika kwa sababu ya mafuta mengi ya petroli yaliyo chini ya ardhi yao.
Eneo la Bara Arabu kwa jumla ni
kilomita mraba
3,191,022, ikiwa Saudia inakalia sehemu nne katika tano ya jumla ya maeneo yake, na sehemu iliyobakia ambayo ni moja katika tano inakaliwa na nchi zilizobakia, zote zikiwepo pembezoni mwa Saudia kwenye bahari ya
Ghuba
ya Uajemi,
bahari ya Kiarabu
na
bahari ya Shamu
.
Nchi zilizoko kwenye bara hili ni:
Sita za mwanzo, zikiwemo kwenye Baraza la Ushirikiano wa Nchi za Ghuba, zina mfumo wa kifalme katika
utawala
wake, na ya mwisho ni Jamhuri ya Yemen.
Nchi hizi zina
historia
ndefu inayorudi nyuma kabla ya kuja
Uislamu
, na
ustaarabu
wa aina mbalimbali ulipatikana katika maeneo ya nchi hizi. Katika ustaarabu mashuhuri wa nchi hizi ni ule ustaarabu wa nchi ya Yemeni, ambao ulikuwa ukijulikana kuwa ni ustaarabu wa
Sabaa
, zama za
Balqis
,
malkia
wa Yemen wakati huo.
Kuna
miji
mingi katika Rasi ya Uarabuni, lakini miji mikuu ya madola mbalimbali ya Rasi ya Uarabuni ni
Riyadh
,
mji mkuu
wa Saudia, ijapokuwa kuna miji mashuhuri na mitukufu katika Saudia kama
Makka
na
Madina
.
Mji mkuu wa Yemeni ni
Sanaa
, lakini mingine muhimu ni
Aden
,
Hudeidah
,
Taez
,
Mukalla
,
Shibam
na
Seyun
.
Ama mji mkuu wa Oman ni
Maskat
, lakini kuna miji mengine mashuhuri yenye tarehe kubwa kama
Salala
,
Sohari
,
Nizwa
na
Rustaq
.
Mji mkuu wa Falme za Kiarabu ni
Abu Dhabi
, na mengine mashuhuri ni
Dubai
,
Sharjah
,
Ajman
,
Ras-al-Khayma
,
Ummul-Quwain
na
Fujairah
.
Kuwait, mji mkuu wake ni
Kuwait
, Qatar mji mkuu wake ni
Doha
, na Bahrain ni
Manama
.
Rasi
ya Uarabuni ina
jangwa
kubwa la
Rub al Khali
kusini mwake na
An-Nafud
kaskazini mwake. Ni sehemu ya
ulimwengu
ambayo haina mvua nyingi na ukame ndio tabia ya nchi zilizokuwemo katika bara hili. Kwa hivyo,
hali ya hewa
huwa ni
joto
sana katika
majira ya joto
kufikia hadi daraja 55
C°
katika baadhi ya sehemu zake, na kufikia daraja hadi 0 C° katika baadhi ya sehemu nyIngine katika majira ya baridi.
Idadi ya wakazi wa nchi hizi saba kwa ujumla inafikia 50,000,000, wakiwemo
asilimia
85 wenyeji na asilimia 15 wageni. Wenyeji au wananchi wa nchi hizi aghlabu yake ni
Waarabu
, lakini pia kuna
Waajemi
,
Mabulushi
,
Wahindi
,
Wabangladeshi
,
Wazungu
,
Wapakistani
,
Waafrika
na
makabila
mengineyo.
Nchi
zote saba zilizoko kwenye Rasi ya Uarabuni ni za
Kiislamu
, na aghalabu Waislamu wake ni wa
madhehebu
ya
Sunni
, lakini pia kuna madhehebu ya
Shia
na ya
Ibadhi
kwenye baadhi ya nchi hizi.
Asilimia 99% ya wananchi wa nchi hizi ni Waislamu, lakini vilevile kati ya wakazi wake, hasa wahamiaji, kuna wafuasi wa
dini
nyinginezo, kama
Wakristo
,
Mabaniani
,
Wayahudi
na kadhalika.
Kiarabu
ndiyo
lugha
inayotumika kwenye nchi hizi saba, na ndiyo lugha rasmi ya nchi hizi, lakini hivi karibuni
Kiingereza
kimeanza kutumika sana kwa sababu ya kuwepo dharura ya kutumia lugha hii katika
biashara
,
mawasiliano
baina ya wananchi na wageni, na katika uhusiano wa kimataifa baina ya nchi mbalimbali ulimwenguni.
Rasi ya Uarabuni ina aina nyingi za
madini
na
nishati
. Kuna
dhahabu
,
fedha
,
chumvi
, na kadhalika. Inajulikana hasa kwa akiba zake kubwa za
mafuta
ya
petroli
na
gesi
, jambo lililofanya hizi nchi kutegemea zaidi maliasili hizi kwa ajili ya kukuza
uchumi
wa nchi zao na
maendeleo
mengine ya nchi.
Hapo zamani watu wa nchi hizi walitegemea sana
uvuvi
,
ufugaji
wa
wanyama
kama
mbuzi
,
kondoo
,
ng'ombe
,
ngamia
na
farasi
. Aidha, walikuwa wakilima na kupanda
mitende
,
matunda
,
ngano
na
shayiri
, na kwa hivyo, bidhaa zao walizokuwa wakisafirisha nje zilikuwa zaidi ni
tende
,
buni
,
samaki
na
papa
wakavu, na
ngozi
za wanyama.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Asia
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Rasi ya Uarabuni
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|