Tunduru ni mji wa Tanzania kusini na makao makuu ya wilaya ya Tunduru katika Mkoa wa Ruvuma . Umbali wake na Songea mjini ni kilomita 272; kwa usafiri wa gari unaweza kutumia muda wa saa 4-5. Jamii inayoishi Wilayani Tunduru ni Wayao , na wanategemea sana shughuli za kilimo cha korosho na sasa wamejikita sana kwenye kilimo cha mpunga . Jamii za wilaya hii inaamini sana katika masuala ya jadi yaani jando na unyago kama njia kuu ya kutolea elimu kwa vijana . Pia jamii hii inakabiliwa na tatizo kubwa la afya kutokana na uhaba wa zahanati .