Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Matunda
ni sehemu za
mimea
zilizo na
mbegu
ndani yao.
Kwa lugha ya
biolojia
ni ovari ya
ua
iliyoiva. Ovulo au chembekike ndani ya ovari zinakuwa mpaka kuwa mbegu. Kwa hivyo hata
kokwa
, matumba ya
maharagwe
,
nyanya
na
matango
ni matunda kwa kibiolojia. Lakini kwa lugha ya kila siku tunda lina nyama tamu au chungu. Nyanya na matango huitwa
mboga
kwa kawaida.
Ukuta
wa ovari huunda ganda la tunda na nyama pia kama iko. Kama nyama hii ina lishe kwa
binadamu
na ladha ya kupendeza basi ni tunda la kuliwa.
Matunda mengi yana
maji
ndani yao pamoja na
sukari
asilia. Asilimia kubwa ya tunda ni
nyuzi
za vitembwe. Ina kiasi kikubwa cha
vitamini
na
madini
kama
chuma
. Kwa kawaida matunda hayana
protini
na
mafuta
mengi isipokuwa matunda ya pekee kama
maparachichi
.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
biolojia
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Tunda
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|