Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mbingu
na purgatorio ya
moto
.
Mchoro
wa
Hannibal Carracci
.
Toharani
(pia
Purgatorio
) kadiri ya
imani
ya
Kanisa Katoliki
ni hali ya
muda
ambayo
huruma ya Mungu
inawatakasa
marehemu
waliofariki
dunia
katika
urafiki
naye lakini bila
usafi
kamili unaotakiwa kwa kuingia
mbinguni
.
Sisi tuliobaki
duniani
tunaweza kuharakisha
utakaso
wao kwa kumtolea
Mungu
sala
na
sadaka
, hasa
ekaristi
.
Yuda Mmakabayo
“alichanga fedha kwa kila mtu jumla drakma elfu mbili, akazipeleka Yerusalemu kutoa sadaka ya dhambi. Kwa kufanya hivi alitenda vema na kwa haki, kwa kuwa aliukumbuka ufufuo wa wafu. Maana kama asingalitumaini ya kuwa wale waliokufa watafufuka, ingalikuwa kazi bure isiyo na maana kuwaombea wafu. Lakini kwa kuwa aliufikiri utukufu wa thawabu waliowekewa wale wafao katika utauwa, wazo lake lilikuwa takatifu na la kicho. Ndiyo sababu alifanya upatanisho kwa wafu ili wafunguliwe dhambi zao” (
2Mak
12:43-46).
Imani hiyohiyo iliongoza
Wakristo
wa kwanza kuwafanyia marehemu
ibada
ambayo haieleweki vizuri, lakini hailaumiwi na
Mtume Paulo
: “Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?” (
1Kor
15:29).
|
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Toharani
kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|