Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Teofilo wa Antiokia
(kwa
Kigiriki
Θε?φιλο? ? ?ντιοχε??, Theofilos o Antiokheus, alifariki
183
/
185
BK
) alikuwa
Patriarki
wa
Antiokia
[1]
baada ya Eros na kabla ya Maximus I
[2]
[3]
.
Kutoka
maandishi
yake (
Eusebi wa Kaisarea
na
Jeromu
walitaja
vitabu
mbalimbali vya Teofilo vilivyokuwepo nyakati zao, ambavyo kati yake kimebaki kile
Utetezi
kwa Autolycus
[4]
,
rafiki
yake msomi lakini
Mpagani
) tunajua kwamba alizaliwa na
Wapagani
katika eneo la
mito
Tigri
na
Eufrate
, na kwamba aliingia
Ukristo
kwa kusoma
Biblia
, hasa
vitabu
vya
kinabii
.
[5]
Kutoka kwa
mwanahistoria
Eusebius wa Kaisarea
tunajua
juhudi
zake za kupinga
uzushi
, hasa ule wa
Marcion
[6]
, akichangia fasihi ya Kikristo, hoja za dini, ufafanuzi wa Biblia na utetezi wa dini.
[7]
Maandishi yake ndiyo ya zamani kuliko yale yote tuliyonayo yanayotaja
Utatu Mtakatifu
.
Tangu kale anaheshimiwa kama
mtakatifu
.
Sikukuu
yake huadhimishwa
tarehe
13 Oktoba
[8]
.
- ↑
Eusebius
,
Ecclesiastical History
iv. 20;
Jerome
Ep. ad Algas. quaest.
6.
- ↑
Henry Fynes Clinton
,
Fasti Romani
- ↑
John Lightfoot
,
S. Ignatius
, vol. ii. p. 166.
- ↑
Jacques Paul Migne
's
Patrologia Graeca
, t. vi. col. 1023-1168 and a small edition (Cambridge 1852) by
W. G. Humphry
.
Johann Carl Theodor von Otto
's edition in the
Corpus apologetarum christianorum saeculi secundi
vol. ii. (Jena, 1861) is by far the most complete and useful.
English translations by
Joseph Betty
(Oxford 1722),
W. B. Flower
(London, 1860),
Marcus Dods
(Clark's
Ante-Nicene Library
), and Robert M. Grant (Clarendon Press, 1970).
- ↑
Apologia ad Autolycum
i. 14, ii. 24.
- ↑
Ecclesiastical History
iv. 24.
- ↑
William Sanday
,
Studia Biblica
, p. 90 describes him as "one of the precursors of that group of writers who, from
Irenaeus
to
Cyprian
, not only break the obscurity which rests on the earliest history of the
Church
, but alike in the East and in the West carry it to the front in literary eminence, and distance all their heathen contemporaries".
- ↑
Martyrologium Romanum
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|