Sully Prudhomme ( 16 Machi 1839 ? 7 Septemba 1907 ) alikuwa mwandishi na mshairi kutoka nchi ya Ufaransa . Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Rene-Francois-Armand Prudhomme. Mashairi yake yanaonyesha sifa za ujumi . Mwaka wa 1901 alikuwa mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Nobel kwa Fasihi .