Mfalme Solomoni
kadiri ya
Biblia
alikuwa mfalme wa tatu na wa mwisho wa
Israeli
nzima, akitawala kuanzia
970 KK
hadi
930 KK
hivi.
Alikuwa mwana wa
Daudi
na Bath-Sheba (
Betsheba
), aliyewahi kuwa
mke
wa
Uria Mhiti
.
Daudi alimchagua kuwa mrithi wake kwa sababu alikuwa uthibitisho hai wa
msamaha
aliopewa na
Mungu
kwa
kuzini
na hatimaye kumuua Uria.
Ufalme wake ulitazamwa na
Wayahudi
kuwa na ustawi usio na mfano, kutokana na
hekima
yake na
amani
iliyopatikana wakati wote wa utawala wake.
Ufalme wake uliweza kustawi kuliko ule wa baba yake kutokana na msingi imara aliouweka Daudi. Lakini mwenyewe aliudhoofisha na kusababisha mara baada ya kifo chake utokee utengano kati ya makabila ya Kaskazini na yale ya Kusini.
Kati ya kazi muhimu alizozifanya, mojawapo ni kujenga
hekalu la Yerusalemu
na kuliweka wakfu kwa sherehe kubwa ya siku saba, ambapo Mungu alionyesha kibali chake kwa kulijaza kwa sura ya wingu (
1Fal
8). Polepole
hekalu
hilo likaja kuwa la pekee hata
patakatifu
pengine pote pakakatazwa chini ya mfalme
Yosia
.
Ingawa Solomoni anasifiwa kwa
hekima
yake, alishindwa kukwepa
majivuno
na
tamaa
, akataka kuwapendeza wake zake waliokuwa 700 (mbali na masuria 300), wengi wao
Wapagani
, hata akawajengea mahali pa kuabudia miungu yao akamchukiza Mungu hata akamtabiria mtoto wake atanyang’anywa sehemu kubwa ya ufalme (1Fal 11:1-13) ikawa hivyo.
Hata hivyo mwishoni aliweza kulaumiwa kwa kuzidisha fahari, hasa upande wa wanawake waliomvuta kwenda kinyume cha
imani
ya
Mungu
pekee.
"Nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako,
na kupambanua mema na mabaya;
maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi"? (1Fal 3:9)
"Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe,
mbinguni juu wala duniani chini!
Ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako,
waendao mbele zako kwa mioyo yao yote". (1Fal 8:23)
Kwa sababu hiyo, ufalme ulivunjika pande mbili mara baada ya kifo chake.
Hata hivyo, Wayahudi waliendelea kumuona kama kielelezo cha hekima, wakaandika vitabu kwa kutumia jina lake au kwa kujifananisha naye.
Yesu
alijitangaza kuwa mkuu na mwenye hekima kuliko Solomoni.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: