Spiro Theodore Agnew ( 9 Novemba , 1918 ? 17 Septemba , 1996 ) alikuwa mwanasiasa wa Marekani . Kuanzia mwaka wa 1967 hadi 1969 alikuwa gavana wa jimbo la Maryland . Halafu alikuwa Kaimu Rais wa Marekani chini ya Rais Richard Nixon kuanzia mwaka wa 1969 hadi 1973 . Alishtakiwa na kugunduliwa kuwa na hatia ya rushwa , akajiuzulu tarehe 10 Oktoba 1973. Rais Nixon akamchagua Gerald Ford amfuate Agnew kama Kaimu Rais.