Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Siprila wa Kurene
(alifariki
Kurene
, leo nchini
Libya
,
300
hivi) ni kati ya
Wakristo
waliouawa kikatili wakati wa
dhuluma
ya
kaisari
Diokletian
.
Alipokataa kutoa
sadaka
kwa
miungu
, walimtia
mkononi
ubani
na
makaa
ya
moto
ili kwa kuvidondosha
altareni
kutokana na
maumivu
aonekane kama kwamba amekubali; kumbe yeye aliyashikikilia
muda
mrefu. Baada ya hapo aliteswa kwa
ukatili
hadi kufa
[1]
.
Tangu kale anaheshimiwa kama
mtakatifu
mfiadini
.
Sikukuu
yake huadhimishwa
tarehe
5 Julai
[2]
[3]
.
Inaonekana ni yule
mjane
Sirila wa Kurene anayeheshimiwa kama mtakatifu mfiadini tarehe hiyohiyo
[4]
. Pengine wanatajwa pamoja naye Aroa na Lusia
[5]
.
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|