Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Siku ya Wanawake Duniani
huadhimishwa
tarehe
8 Machi
ya kila
mwaka
. Siku hiyo ilianza kuadhimishwa tarehe 8 Machi
1975
baada ya
Umoja wa Mataifa
kuridhia siku hii kutumika
[1]
kama siku rasmi ya kuikumbusha
dunia
juu ya
haki
za
wanawake
.Siku hii pia huongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume katika jamii. Aidha maadhimisho ya siku hiyo kwa mwaka huu yamebeba ujumbe wa usawa kwa watu wote.
Historia
Siku ya wanawake duniani kwa mara wa kwanza ilisherehekewa katika mwaka wa
1911
ambapo mataifa
kumi na moja
yalikusanya wanawake mia moja walipoanza kuadhimisha siku hii.
Mwaka
1908
jumla ya wanawake elfu kumi na tano waliandamana katika katika
mji
wa
New York
wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi ,kupata
ujira
wa kuridhisha na kupewa haki ya kupiga
kura
[2]
.
Mwaka
1909
mwanamke kwa jina la
Clara Zetkin
alipendekeza kuanzishwa kwa siku ya wanawake duniani katika mkutano wa
wafanyakazi
wanawake uliofanyika katika jiji la
Copenhagen
nchini
Denmark
.
Marejeo