Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
sarafu ya KSh 10
Shilingi ya Kenya
(
KES
au
Ksh
) ni
fedha
za
Kenya
. Shilingi moja imegawanywa kwenye senti mia moja.
Shilingi ya Kenya ilianzishwa mwaka 1966 baada ya kuvunjwa kwa bodi ya fedha ya Afrika ya Mashariki iliyosimamia fedha ya pamoja ya Kenya,
Tanzania
na
Uganda
iliyoitwa
East African Shilling
iliyotumiwa katika maeneo yote yaliyokuwa chini ya Uingereza katika Afrika ya Mashariki.
Kuna
sarafu
za shilingi 1, 5, 10, 20 na 40.
Sarafu za senti zipo za zamani za senti 1, 5, 10, 20 na 50 lakini hazinunui kitu tena.
Noti
zilitolewa za shilingi 5, 10, 20, 50, 100, 200, 500 na 1000 ingawaje noti za shilingi 5, 10 na 20 ni nadra sana kuonekana.
Majina ya zamani:
- Thumuni 1 = Senti 50
- Peni 1 = Senti 10
- Ndururu 1 = Senti 5
Sarafu
-
Sarafu ya shilingi 5 - mbele
-
Sarafu ya shilingi 5 - nyuma
-
Sarafu ya shilingi 10
-
Sarafu ya shilingi 20
-
Sarafu ya shilingi 40 (ilitolewa miaka 40 baada ya uhuru)
Benknoti
Benknoti za Kenya 2010
|
Picha
|
Thamani
|
Ukubwa kwa milimita
|
Rangi
|
Maelezo
|
Mbele
|
Nyuma
|
Mbele
|
Nyuma
|
Alama
|
|
|
50
|
138 × 72
|
Kahawia-Kijani
|
Picha ya
Jomo Kenyatta
|
Sanamu ya ndovu,
Mombasa
, Ngamia
|
Simba
|
|
|
100
|
141 × 74
|
Dhambarau-Kijani
|
Kenyatta International Conference Centre
na sanamu ya Kenyatta,
Nairobi
|
|
|
200
|
144 × 76
|
Kijivu-kijani
|
Mavuno ya pamba
|
|
|
500
|
147 × 78
|
Kijivu-kijani
|
Jengo la bunge mjiniNairobi
|
|
|
1000
|
150 × 88
|
Kahawia-kijani
|
Tembo na nyati
|
|
Makala hii kuhusu mambo ya
uchumi
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Shilingi ya Kenya
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|