Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sevilla
ni mji mkubwa kando la mto
Guadalquivir
katika kusini ya
Hispania
na mji mkuu wa jimbo la kujitawala la
Andalusia
mwenye wakazi 700,000.
Mji ulianzishwa zamani za
Wafinisia
ukaendelea kukaliwa na kutawaliwa na
Waroma wa Kale
,
Wavandali
halafu na
Wavisigothi
na tangu
711
na Waarabu Waislamu. 1248 ulivamiwa na wafalme wa
Kastilia
na kubaki upande wa Hispania ya kikristo.
Majengo mengi mazuri yanatunza kumbukumbu ya historia hii. Boma la Alcazar lilijengwa na mafundi waislamu kwa niaba ya wafalme wakatoliki. Sevilla ilikuwa na ofisi kuu ya utawala kwa koloni za Hispania katika Amerika.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Hispania
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Sevilla
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|