Senati
(pia
Seneti
kutoka
Kiingereza
"Senate") ilikuwa
baraza
kuu katika
Dola la Roma
.
Jina
lake limetokana na
neno
la
Kilatini
senes
(=
mzee
), kwa hiyo senati ilikuwa baraza la wazee ("Senatus").
Wakati wa
Jamhuri ya Roma
senati ilikuwa chombo kikuu cha
dola
; wakati wa
makaisari
tangu
Augusto
umuhimu wake ulipungua lakini kwa muda mrefu makaisari walijitahidi kuheshimu baraza hilo hata kama
mamlaka
zake zilipungua zaidi na zaidi.
Sheria
zilitangazwa kwa jina la senati; wakati wa fitina kati ya senati na
mtawala
kulikuwa pia na
amri
za Kaisari zilizotangazwa bila idhini ya senati, lakini kwa jumla makaisari hawakutumia jina "sheria" kwa amri hizo.
Kimsingi senati ilijumlisha wote waliowahi kuwa
maafisa
wakuu wa dola. Katika utaratibu wa Kiroma maafisa wote walichaguliwa kwa muda wa
mwaka
mmoja. Wenye
vyeo
hawakupata
mishahara
, kwa hiyo walikuwa hasa
matajiri
walioweza kugombea nafasi hizo. Kwa sababu hiyo senati kama mkutano wa maafisa wa kale ilijumlisha hasa watu kutoka
familia
za
makabaila
au familia tajiri nyingine.
Wakati wa Jamhuri ya Kiroma senati ilikuwa na maseneta 100 walioongezeka baadaye kuwa 300.
Gaius Julius Caesar
aliongeza vyeo hivi hadi wajumbe 900.
Senati ilidumu hadi mwisho wa Dola la Roma. Katika
Dola la Roma Magharibi
heshima yake ilikubaliwa ndani ya
mji
wa
Roma
tu na habari za mwisho wa senati zimepatikana hadi mwaka
600
BK
. Katika
Dola la Roma Mashariki
(
Bizanti
) senati ilidumu hadi mwisho kabisa, mnamo mwaka
1453
, lakini
karne
za mwisho haikuwa na athira yoyote.
Senati ya Roma ilikuwa mfano kwa nchi nyingi; katika
lugha
za Ulaya
taasisi
mbalimbali huitwa kwa jina hili.
Senati kama kitengo cha bunge katika nchi mbalimbali
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Nchi mbalimbali huwa na senati kama sehemu ya
bunge
ikiwa ni bunge ya vitengo viwili (
nyumba
mbili
au vyumba viwili); hapo "senati" kwa jumla ni jina la "nyumba ya juu".
Katika
Marekani
"
Senati
" ni kitengo kimoja cha
bunge
ikiwa na mamlaka nyingi kuhusu
siasa ya nje
na kuthibitishwa kwa maafisa wakuu wa
serikali
.
Rais
anahitaji kibali cha senati kwa sehemu muhimu za
siasa
zake. Senati ya Marekani inaweza kusimamisha sheria zilizoamuliwa na
Nyumba ya Wawakilishi
(sehemu nyingine ya bunge). Senati ina wajumbe wawili kutoka kila
jimbo
la Marekani wanaochaguliwa kwa muda wa miaka 6.
Sawa na Marekani, kuna "Senati" kama kitengo cha bunge katika
Ufaransa
,
Kanada
,
Italia
(Senato della Repubblica),
Rumania
,
Ucheki
,
Hispania
(Senado),
Poland
,
Ubelgiji
,
Australia
,
Kenya
na
Brazil
.
Nchi nyingine zenye bunge la vitengo viwili hazitumii neno "senati", kwa mfano
Ujerumani
. Nchini Ujerumani "senati" ni jina la vitengo vya
mahakama kuu
.
Katika nchi mbalimbali "Senati" ni jina la baraza kuu kwenye
chuo kikuu
.